Kwanza ilikuja mechi ya lazima kushinda dhidi ya Valencia katika Champions league hatua ya makundi. Kama Chelsea wangeshindwa kuwafunga Valencia, wangejikuta nje ya michuano ya ulaya.
Then ikafuatia hatua ya 16 bora dhidi Napoli. Katikati ya kipindi ambacho walikuwa wakifanya vibaya sana msimu huu, Chelsea walifungwa vibaya sana na Napoli nchini Italy, 3-1.
Lile goli la ugenini liliwapa Chelsea matumaini, ingawa, chini ya kocha mpya Roberto Di Matteo, Chelsea waliweza kucheza vizuri na kupata ushindi dhidi ya Napoli katika mechi ya pili iliyowapeleka katika robo fainali.
Walipofika nusu fainali, hata mashabiki wa Chelsea walijitaarisha dhidi ya maumivu ya kutolewa. Waliona hakuna jinsi Chelsea wataweza kuwahimili katika dakika 180 za hatua hiyo.
Lakini Chelsea walifanya kile kitu ambacho timu nyingi ikiwemo Rea Madrid huwa ni taabu au hushindwa kabisa kufanya - kuwafunga Barcelona.
Kwa bahati mbaya zaidi katika mapambano ya kufika hapa walipo Chelsea wamewapoteza wanajeshi wao muhimu ambao wanaufanya mchezo wa fainali dhidi ya Bayern Munich uwe mgumu sana kwao.
Haya baadhi ya mambo kadhaa yatakayoipa ugumu Chelsea dhidi ya Bayern Munich pale Allianz Arena.
UKUTA DHAIFU
Katika wachezaji wote wa Chelsea waliosimamishwa wakati wa mchuano wa kuelekea fainali, Branislav Ivanovic anaweza akaa mtu mgumu sana kumpatia mbadala wake.
Huku John Terry akiwa amesimamishwa na Gary Cahil akiwa majeruhi, David Luiz ni beki wa kati pekee ambaye kwa uhakika anaweza akawepo katika fainali lakini naye pia ndio kwanza ametoka kupona majeraha.
Je Gary Cahil ataweza kupona na kucheza katika fainali? Kama ndio, je ni kiasi gani atakuwa na match fitness? kama atakuwa hayupo sawa nani atacheza katika nafasi yake?
Chelsea walikuwa na mabeki wao wote katika nusu fainali ya Chmpions league kitu ambacho kiliwasaidia kucheza vizuri dhidi ya Barca.
Huku wakiwa wanawakosa atleast mabeki wao tegemeo wawili au watatu katika fainali, napatwa na wasiwasi ni namna gani wataweza kuhimili kasi ya Arjen Robben, Frank Ribery and Mario Gomez na kuwazuia wasiwadhuru.
KUTOKUWEPO KWA RAMIRES
Je Chelsea wangeweza kuifunga Barcelona bila uwepo wa Ramires?
Sidhani, kama wangeweza. Mbrazil huyu alikuwa mhusika mkuu katika upatikanaji wa magoli mawili katika mechi ya kwanza na ya pili kabla ya Fernando Torres kuongeza barafu kwenye cake.
Na ndio maana bila kuwepo kwake kunaleta shida kifogo katika safu ya kiungo ya timu ya Chelsea - ukizingatia Ramires ndio roho ya safu ya kiungo ya The Blues, akikaba na kushambulia bila kuchoka.
Ingawa sio mchezeshaji, lakini Ramires ni mchezaji mwenye kariba ya aina yake, hata inapotokea Chelsea wanapokuwa kwenye presha kubwa na kutoweza kukaa na mpira muda mrefu, yeye ni mchezaji ambaye hung'ara na kuleta impact fulani, tofauti na Juan Mata.
Ivanovic ataiumiza safu ya ulinzi ya Chelsea, lakini naamini kutokuwepo kwa Ramires kunamuumiza zaidi kichwa Roberto Di Matteo ikizingatiwa hata Raul Meireles nae hatakuwepo kwa mchezo huo huku Essien kiwango bado kikiwa hakipo swa kutokana na majeruhi ya muda mrefu.
UCHOVU
Chelsea wana ratiba ngumu sana mwishoni mwa msimu.
Kutoka sasa mpaka May 13, hakuna wiki ambayo Chelsea hawatocheza mechi mbili. Huku wakiwa wanaitafuta nafasi mojawapo kati ya nne za juu, Roberto Di Matteo atahitaji kuendelea kupanga kikosi imara katika michezo ya ligi iliyobakia.
Hili linamaanisha kwamba wachezaji wa Chelsea watakuwa wamechoka wakati wa mchezo wa fainali utakapowadia mwezi ujao May 19.
Bayern Munich wana unafuu kidogo katika ratiba yao, ligi ya kwao imeshaisha na wameshapoteza ubingwa kwa Dortmund na tayari wamejihakikishia moja ya nafasi 3 za kucheza Champions league - hivyo tofauti na Chelsea wenyewe wana uwezo kufanya rotation na kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wao muhimu kwa ajili ya kuwasubiri Chelsea pale uwanjani kwao wenyewe Allianz Arena.
MBINU
Naamini hata kama Chelsea wangekuwa na mabeki wao wote wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo wa fainali dhidi ya Bayern Munich - mbinu yao ya kupaki basi haitokuwa nzuri dhidi yao.
Tofauti na Barcelona, Bayern Munich wana mshambuliaji bora wa kati ambaye kwa sasa yupo on fire tayari Mario Gomez. Hivyo hawategemei kufunga magoli kwa mipira ya chini tu - wanaweza wakatumia krosi kumtengenezea Gomez magoli.
Naamini baada ya krosi kadhaa katika kichwa cha Gomez, basi yeye au Thomas Mueller wanaweza wakaipa uongozi Bayern katika mechi hiyo.
Cha kuongezea, Arjen Robben na Bastian Schweinsteiger, na Ribery wote wanaweza kupiga mawe - mashuti ya mbali. Kupaki basi kwa Chelsea kutawapa nafasi ya kufanya hivyo mara nyingi - na moja kati ya hayo yanaweza kumpita Cech na kuishia ndani ya nyavu.
Huna lolote wewe, kila mara unajifanya mchambuzi lakini uchambuzi wako unaishi kuwa hakuna lolote...tatizo unakuwa so bias, watu kama kina Phil McNulty, Pat Navin kila mara wako fair sana, than kuangalia upande mmoja, juzi kabla ya game la Barcelona uchambuzi ulikuwa kama wa leo, hivi vile, wewe chambua za Simba, Yanga na Azam...huna lolote jipya.
ReplyDeleteMdau
Washington
Kaka kila siku unatupa nafasi finyu halafu tunakuumbua na mitazamo yako ya upande mmoja kila siku.huchoki 2 kaka.
ReplyDeleteUlisema hivyo hivyo tukawang'oa barca! hilo lisikupe shaka the blues ndo yetu ile pole shaffih
ReplyDelete