Search This Blog

Thursday, April 19, 2012

KWANINI PAUL SCHOLES NDIO KIUNGO BORA KUWAHI KUTOKEA KATIKA ZAMA ZA PREMIER LEAGUE.


Cesc Fabregas, Frank Lampard, Steven Gerrard, Claude Makelel, Roy Keane na Patrick Vieira - wote ni viungo wakali waliowahi kutokea katika premier league, lakini sio category ya kiungo wa Manchester United - legend Paul Scholes.

Premier league sasa ina umri wa miaka 20 - na kumekuwepo na mjadala nani ni kiungo bora ambaye wanadhani amewahi kucheza katika ligi hiyo tangu ilipoanza katika mwaka 1992.

Watu wengi wakiwemo wachezaji na wachambuzi wa soka wamekuwa wakimtaja Paul Scholes kama kiungo bora kuwahi kutokea katika ligi hiyo.

Wakati candidates wengine, kama mchezaji wenzie wa zamani wa Roy Keane na Paul Ince, Fabregas, Gerrard, Lampard, Makelel, Matt Le Tissier na Emmanuel Petit walikuwa maestro wa hatari katika safu ya kiungo, lakini hakuna ambaye ana impact ya Scholes.

Kwa hili ni mchezaji ambaye anastahili kabisa kuitwa kiungo bora kabisa kuwahi kutokea katika premier league.

Katika miaka yote 19 ya kucheza soka katika level ya juu, Scholes ameshinda medali nyingi sana.

Na wakati akiwa mtu mwenye kuona sana aibu mbele ya vyombo vya habari, wale ambao walicheza nae au walicheza dhidi yake wamekuwa ndio wasemaji wa kipaji chake.

Thierry Henry: "Manchester United siku zote wamekuwa na wachezaji wazuri, lakini wakati wowote tulipokuwa tunakutana nao, siku zote nilikuwa naogopa kitu ambacho Paul Scholes atafanya.
Muulize mtu yoyote kutoka katika kikosi cha zamani cha Arsenal, watakuambia haya ninayokuambia.
Ikiwa utamuachia acheze, anaweza kukuua, na mimi najua wengi walikuwa wanamuona wa kawaida. Jinsi alivyokuwa akicheza, pasi moja, huku akiwa mtu wa mwisho kufika katika box, jinsi anavyopiga mashuti, muono wake, na pasi zake- alikuwa hatari sana.
Najua watu wamekuwa wakimsema kwwa tackling zake, lakini mimi nilipenda vile. Anajua namna ya ya kuipeleka timu mbele na kutuliza mashambulizi ya wapinzani. Kwangu mimi ni mmoja ya viungo bora kabisa ambao nimewahi kuwashuhudia maishani mwangu."

Na kama hiyo haitoshi, haya ndio aliyoyasema Xavi Hernandez - kiungo wa FC Barcelona ambaye wengi tunaamini ndio mpiga pasi bora duniani - aliyasema kuhusu mchezaji ambaye mara kwa mara amekuwa akimuongelea kwa pamoja na Xabi Alonso.

"Katika miaka 15 mpaka 20 iliyopita kiungo bora ambaye nimewahi kumshuhudia - ambaye amekamilika ni Paul Scholes. Nimeongea na Xabi Alonso kuhusu Scholes mara nyingi sana. Ni MCHEZAJI HATARI NA AKILA KITU.

Anaweza kucheza pasi ya mwisho, kufunga, ana nguvu, ni vigumu sana kumpora mpira na vigumu kuupoteza. Kama angekuwa Hispania then labda angekuwa amethaminiwa zaidi."

In fact, Zinedine Zidane,(ambaye alimuita Scholes mpinzani wake mkubwa) Socrates, Marcello Lippi, Laurent Blanc, Bobby Chalrton, Edgar Davids, Cesc Fabregas, Ryan Giggs wote wamekuwa wasemaji wakubwa wa uwezo na kipaji cha Scholes.

Tumesikia na kusoma mengi kuhusu wachezaji na makocha wengine wakimsifia Paul Scholes kama kiungo bora, lakini sababu kubwa kwanini ni kiungo bora tokea premier league ianzishwe inaangukiakatika msimu wa sasa akiwa na klabu yake ya Manchester United - ambayo alijiunga nayo tena miezi sabab baada ya kuamua kustaafu.

Tangu arudi dimbani kumsaidia boss wake na rafiki yake wa zamani Sir Alex Ferguson, Scholes ametoa msaada mkubwa ambao hata mashabiki wake wakubwa wasingwahi kufikiri.

Kurudi kwake katika kikosi cha Manchester United kumueleta tofauti kubwa ndani ya kikosi hicho ambacho tangu kuumia kwa Tom Cleverlley mwanzoni mwa msimu kulileta hali tete ndani ya timu hiyo hasa katika safu ya kiungo.

Msimu huu, Scholes ana wastani wa 9.9 wa kupiga mipira mirefu kwa mchezo na pasi zimefika kwenye target kwa wastani wa asilimia 92.5.

Hilo linamfanya ashike namba mbili katika listi ya  wapiga pasi nyingi zilizofanikiwa katika premier league - nyuma ya Leon Britton wa Swansea City, inashangaza - lakini Britton anapiga wastani wa 4.2 ndogo kuliko za Scholes kwa mechi.

Na katika sula la kusambaza mipira, hapo ndio anakamata usukani kwa kufanya hivyo - Mchezaji wa Tottenham na kiungo mchezeshaji Luka Modric anashika nafasi ya pili kwa sasa, akiwana wastani wa 7.5 wa kupiga mipira mirefu kwa mechi.

Lakini pamoja na kupiga sana pasi, Scholes pia amekuwa akifunga - bao lake la kwanza tangu arudi kutoka kustaafu alifunga katika mechi dhidi Bolton Wanderes, kabla ya kufunga bao muhimu katika mechi dhidi ya Norwich City, kabla ya kuwamaliza Queens Park Rangers.

Haya yote ameyafanya mchezaji ambaye katika nusu ya kwanza ya msimu alikuwa akiishi maisha ya mcheza soka mstaafu, akifanya mazoezi na timu za vijana katika klabu yake ili aweze kuwa fiti.

Hili linadhihirisha kwamba uwezo na kipaji cha Paul Scholes hakitopotea.
Tumeshuhudia nini kinatokea kwa wachezaji kama Roberto Pires na Robbie Fowler walipojaribu kuongeza muda wa kucheza soka walipofika umri mkubwa- walifeli.

Scholes akiwa na miaka 37, bado anacheza soka la kiwango cha juu, huku bado akiwa na umuhimu mkubwa katika klabu kubwa ya Manchester United.

Hakuna mchezaji yoyote katika premier league au duniani katika soka, angeweza kucheza soka la kiwango juu analocheza Scholes tena akiwa katika umri mkubwa wa miaka 37, tena hasa baada ya kukaa nje ya game kwa miezi saba bila kucheza soka la ushindani.

N a ndio maana Paul Scholes anastahili kuitwa mchezaji bora wa muda wote katika zama za premier league katika safu ya kiungo.

Ndio mchezaji ambaye amedumu katika soka la kiwango cha juu kwa muda mrefu kuliko wote duniani, tena hasa katika premier league na pia ni mmoja ya role models katika michezo duniani.

Roy Keane anatufungia mjadala huu kwa kusema: "Hakuwa na mbwembwe za umaarufu, hakujitangaza lakini ndio mchezaji aliyebarikiwa na kubakia kutodhurika na udhaifu unaotokana na ubinadamu."

1 comment: