Miezi kadhaa iliyopita niliripoti kwamba mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba kutoka Kenya Jerry Santo amepata timu ya kuichezea nchini Albania ya KF Tirana - kabla ya hivi karibuni kutoka kwa taarifa kwamba hatoweza kuichezea tena timu hiyo tena.
Sasa nikiwa hapa Kenya Jerry Santo amenieleza kiundani kilichosabaisha asiweze kuichezea KF Tirana ambayo tayari ilishatangaza kumsajili mapema mwaka huu.
"Kiukweli nilishasajiliwa na kupewa mkataba wa miaka 2 na ile timu, lakini nikiwa katika maandalizi ya kujiunga nayo yakafanyika mabadiliko makubwa katika uongozi wa klabu ile ambayo yaliutoa uongozi ulionisajili ndani ya timu ile. Uongozi mpya ulipoingia madarakani nao ukafanya baadhi ya changes ndani ya timu hiyo - kwanza baadhi ya wachezaji wapya tuliosajiliwa na uongozi wa zamani mikataba yetu wote ikavunjwa. Hivyo hicho ndicho kilichotokea mpaka nikashindwa kucheza soka kule."
Vipi je upo tayari kurudi Simba ikiwa watakuhitaji?
"Nipo tayari kurudi Simba, ni timu ambayo naipenda na kuitahmini. Nina marafiki wengi pale na nina maelewano mazuri na uongozi wa klabu ile. Pale sasa ni kama nyumbani ikiwa watanihitaji nitarudi kuitumikia Simba." - amesema Santo ambaye bado ana ndoto za kwenda kucheza soka nje ya Afrika.
No comments:
Post a Comment