Ilionekana ni rafu ambayo ilijaa visasi vitupu - rudisha kumbukumbu zako nyuma katika dakika ya 93 ya fainali ya Carling Cup ya 2007 kati ya Chelsea na timu ya zamani ya Fabregas Arsenal.
Kikosi cha Jose Mourinho walikuwa wanaongoza 2-1, then Kolo Toure wa Arsenal akivamiana na Jon Mikel Obi. Waafrika hao wawili ndio waliogongana, lakini Lampard na Fabregas wenyewe ndio walikuwa wa kwanza kufika katika eneo la tukio.
Lampard akakabilaina na Toure, Fabregas akaja akamvuta kiungo huyo wa England kwa nyuma kwa kumvuta shingo yake na ukazuka utata mkubwa. Howard Webb aliwatoa Toure, Mikel na Emmanuel Adebayor kabla ya Chelsea kubeba kombe.
Chanzo cha Ugomvi |
Na hapo ndipo ugomvi kati ya wachezaji hawa wawili ulipoanza - tangu wakati huo wameshakutana uwanjani mara 18.
Mchezaji mwenzie Fabregas wa Arsenal Jack Wilshare aliandika kupitia mtandao wa Twitter kabla ya mchezo wa kwanza: "Nafikiri Cesc atapenda afunge usiku wa leo . . . . . yeye na Lampard hawajawahi kuwaiva chungu kimoja kwenye dimba."
Ishara ya kwanza ya kutokuelewana kati ya wawili hao ilionekana Jumanne iliyopita mapema kipindi cha pili wakati Fabregas alipoukamata mguu wa Lampard kwa nguvu na kiugomvi huku akiwa amedondoka chini akitaka apewe free kick baada ya tackling ya Lampard.
Hilo likamfanya Wilshare aandike tena: "Niliwaambia nyie Lampard na Cesc sio marafiki kabisa."
Muda mchache baadae Lampard akapewa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Fabregas.
No comments:
Post a Comment