Search This Blog

Wednesday, April 4, 2012

HATIMAYE SAMUEL ETO'O AFUTA KESI YA MADAI DHIDI YA BARCELONA


Straika wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Eto'o ameamua kufuta kesi yake ya madai ya mabilioni ya shilingi dhidi ya klabu yake ya zamani, Barcelona.

Eto'o alikuwa akiida klabu hiyo wakati akihama kwenda Inter Milan ya Italia. Katika madai yake, Eto'o alitaka kulipwa kiasi cha Dola za Kimarekani 3.9milioni kama sehemu ya makubaliano alipohama na kwenda kujiunga na Inter katika msimu wa mwaka 2009.

"Barcelona ingependa kutoa taarifa ya kumshukuru Samuel Eto'o kwa dhamira yake ya kumaliza suala lililokuwa mbele
yetu," ilisema taarifa ya klabu hiyo jana jioni.

"Yeye (Samuel) alikuwa mmoja kati ya wafungaji hodari zaidi kwenye historia ya klabu."
"Klabu imefurahishwa na mchango wake mkubwa wakati wote akicheza hapa, hivyo kwa hatua aliyofikia tunapenda kumshukuru kwa kufika uamuzi huo," ilisema zaidi taarifa ya klabu hiyo.


Nahodha hiyo wa timu ya Taifa ya Cameroon, maarufu kama 'Indomitable Lions', kwa sasa anacheza klabu tajiri ya Russia inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini huo Anzhi Makhachkala.
Alijiunga na Inter katika utaratibu wa kubadilishanawachezaji, ambapo mwenzake Zlatan Ibrahimovic alikwenda Barca. 

Ibrahimovic, nyota wa kimataifa wa Sweden kwa sasa anacheza AC Milan, ambako alikwenda kujiunga kwa ada ya Dola za Kimarekani 61milioni, wakati Eto'o alijiunga na Inter kwa dola 26milioni.

Eto'o alifungua madai yake akitaka kulipwa asilimia 15 ya mauzo yake kwenda Inter. Hata hivyo, Barca ilisema malipo ya asilimia 15 yalikuwa halali kwa wachezaji wale ambao uhamisho wao hakuwa nje ya Hispania.

No comments:

Post a Comment