Katika hatua nyingine Pep Guardiola amejiweka mbali na nafasi ya ukocha pale Stamford Bridge baada ya kuthibitisha kwamba ataondoka Barcelona mwsihoni mwa msimu.
Uamuzi wa Guardiola kuondoka Barca ulizidisha tetesi kwamba atachukua nafasi ya Andre Villas Boas pale darajani msimu ujao - ingawa akiongea wakati wa mkutano waandishi wa habari leo hii Guardiola alisema hana mpango kufanya kazi ya ukocha darajani kwa sababu amepanga kupumzika.
"Sijawahi kukutana na Roman Abramovich au mwakilishi yoyote wa Chelsea. Sihitaji kufundisha soka kwa sasa. Ninahitaji kufanya vitu vingine kwa sasa, labda baadae huko mbeleni naweza kurudi katika benchi la ufundi - lakini kwa sijajua bado.
"Sina chochote cha kuonyesha, na wala sidhani kama nahitaji kwenda nje ya nchi hii ku-prove chochote, ninachohitaji kwa sasa ni kukaa mbali na soka."
Kujiondoa kwa Guardiola katika mbio za kutaka kumrithi AVB kunazidi kuimarisha nafasi ya Roberto Di Matteo kupewa kazi ya moja kwa moja baada ya kuifikisha timu hiyo katika fainali ya Champions league huku wakiwa bado wanaisubiri Liverpool katika fainali ya kombe la FA.

No comments:
Post a Comment