TIMU za vijana wenye umri chini ya miaka 20 za Azam Fc na Simba keshokutwa zinatarajiwa kukwaana katika dimba la Chamazi ikiwa ni mchezo maalum wa kuadhimisha kifo cha rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Aman Karume.
Msemaji msaidizi wa Azam FC Jaffer Idd Maganga alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanakwenda vizuri.
Alisema timu hizo ambazo zimekuwa zikichuana vikali katika michuano mbalimbali ya Vijiana ikiwemo ile inayoshirikisha timu za Vijana ‘Uhai Cup’ ambapo Simba inashikilia ubingwa.
Katika hatua nyingine kikosi cha Azam Academy pamoja na Simba B ni miongoni mwa timu 94 zilizotuma maombi ya kushiriki michuano ya kombe la Muungano inayoshirikisha timu mbalimbali za soka toka pande zote za Tanzania
No comments:
Post a Comment