Kaka Shaffi Dauda hivi ni vituko vya mpira wa mkoa wa Tanga ambavyo vinendelea kwa lengo ya kuibeba African Sports, na vilitokea tarehe 11/03/2012 katika kiwanja cha CCM Mkwakwani Timu hiyo kongwe inayobebwa ilicheza dhidi ya Segera FC. Mchezo hou ulianza kama kawaida saa 10.00 lakini ili kuwa tayari imepangwa kwa lengo lakuibeba hiyo timu kongwe iwe bingwa wa mkoa wa Tanga na ili hitaji kushinda sio chini ya goli 6 – 0 ili imzidi anaeongoza ligi hiyo Small Prison ambaye anaongoza ligi hiyo katika kundi lake. Mwamuzi wa mchezo huo alikuwa ni Ishaka Shirikisho mpaka dk 38 kipindi cha kwanza matokeo yalikuwa 3 – 0 A/Sports ikiwa inaongoza magoli yote hayo Kaka yalikuwa yakuotea mimi ninaeandika ni kiongozi wa Timu ya Raidon F.C ya hapa wilaya ya Tanga, lakini kwa vile ilikuwa imepangwa aliamua kuachia ili wakamilishe idadi ilio takiwa uwezo wao ni mdogo.
Segera FC baada ya kufungwa goli la tatu (3) walilalamika sana na kuamua kutokuendelea na mchezo lakini kilichotokea kwa kuona kuwa tayari matokeo yameshapangwa yawe hivyo, wakaamua kujikusanya pamoja katikati ya kiwanja bila kuendelea na mchezo na walikaa chini wote. Mwamuzi Ishaka Shirikisho kwa kuona hivyo na lengo lake yeye pamoja na “TRFA” kutokamilika alisuburi dk 15 ili wachezaji waje waanze mpira baada ya kuona hawaji na dk kukamilika akamaliza mchezo, na matokeo hayo bado A/Sports hayajamsaidia lakini atabebwa kwa njia nyingine nina uhakika litafanyika na utalisikia.
Kaka Shaffi sio rahisi kwa kiwango cha mpira kwa Tanga na Tanzania kwa ujumla kupanda kitazidi kudidimia, nyinyi watu wa Sports Extra mutapiga kelele sana mwisho mtachoka hakuna kitakachobadilika kwani viongozi wanaingia madarakani kwa maslahi yao, binafsi sisi leo makatibu wa wilaya wa chama cha mpira ndio tunaokaa milangoni kwa lengo la kumbeba mfalme fulani anayetaka madaraka katika mkoa huu, pia kuna Viongozi ambao hawana hata sifa moja ya kuwa viongozi wa mpira wa miguu lakin wapo ni miaka mingi sana nauwezo wao ni mdogo CHANETA ameshindwa, Chama cha mpira wanawake ameshindwa lakini sasa anatakaukatibu mkuu kwa nguvu na ndie anaekaimu sasa hivi na ndio wanaochafua ligi yote hii ambayo inaendelea sasa hivi kwa ajili ya kutaka madaraka tu.
“Mimi mdau wa soka mkoa Tanga”
2. rufaa
AIR SHOOTING FOOTBALL CLUB
Air Shooting Footbal Club,
Sanduku la Posta 413,
TANGA, Machi 2012.
Katibu Mkuu,
Cahama cha Mpira wa Miguu (M) Tanga,
Sanduku la Posta 122,
TANGA, Tanzania .
Yah: Kukata Rufaa Dhidi ya Mchezaji
Pera Ramadhani Mavuo wa African Sports
Ndugu,
Husika na kichwa cha habari hapo juu.
Mchezaji tuliyemtaja hapo juu alichezea timu ya African Sports dhidi ya
Air Shooting siku ya tarehe 06 Machi 2012 akiwa amevaa jezi nambari 11. Mchezaji huyo si halali kuchezea African Sports kwa sababu yeye ni mchezaji halali wa J.K.U FC ya Zanzibar, ushahidi kivuli cha leseni iliyoambatishwa.
Mchezaji huyo alikuwa Zanzibar kwa muda mrefu sana na alianza kucheza timu ya Mundu F.C mwaka 2006 hadi 2009 alipohamishwa Mundu F.C na kuhamia J.K.U FC ya Zanzibar. Ushahidi wa hilo alishiriki katika Kombe la Shirikisho Barani Africa kati ya timu ya Mundu FC na Mwana Africa ya Zimbabwe akiwa na leseni nambari 2978 ya CAF, mwaka 2008 alicheza tena timu hiyo hiyo ya Mundu katika Kombe la Shirikisho Barani Africa dhidi ya timu ya Red Heroes ya Zambia akiwa na leseni nambari 2978 ya CAF, uthibitisho wa hilo Katibu wa ZFA Ndugu Masoud Attai Mobile No. 0777421269 atathibitisha.
Pia Decemba 2009, alisajiliwa na timu ya J.K.U ya Zanzibar ambao walimuhamisha kutoka MUNDU FC na akiwa na leseni nambari 4717 imeambatishwa kama kielelezo, Lesseni hiyo ndio inayotumika hadi leo hii katika Ligi Daraja la kwanza Zanizibar, ushahidi ni mechi alizocheza mwaka 2011/12 na mechi alizocheza ni kama zifuatazo:-
a. Tarehe 21 Octoba 2011 J.K.U V/S Ngome – Uwanja wa Ngome.
b. Tarehe 03 Decemba 2011 J.K.U V/S Bandari – Uwanja wa Ngome.
c. Tarehe 28 Decemba 2011 J.K.U V/S Kijichi – Uwanja wa Ngome.
Ushahidi wa hili Katibu wa J.K.U FC Ndugu Ally Bamba Mobile No. 0777412593 atathibitisha.
Tunaomba tupatiwe ushindi wa mechi hiyo kutokana na timu ya African Sports FC kukiuka kanuni za ligi hiyo kwa kumchezesha mchezaji asiye halali kwao.
Ni matumaini yetu haki itatendeka.
Ahasante
Wako katika Michezo
_________________________
(Mbwana Salum Ally)
Katibu Air Shooting
3. majibu ya rufaa
TANGA REGIONAL FOOTBALL ASSOCIATION
P.O. BOX 122, Mobile: 0754 301033
TANGA – TANZANIA
KUMB No. TRFA/KM/KL/15/012. 13/03/2012
RUFAA YA AIR SHOOTING SPORTS CLUB DHIDI YA
AFRICAN SPORTS CLUB KUPINGA KUCHEZESHWA
MCHEZAJI PERA RAMADHANI MAVUO KATIKA
MCHEZO WA 06/03/2012
Baada ya kupitia vielelezo vyote kamati ya Rufaa imeamua kuwa haina uwezo kisheria na kikanuni kujadili Rufaa hiyo kwani Rufaa hiyo inagusa uhamisho katika ngazi ya kitaifa kati ya TFF (Tanzania Football Association) na ZFA (Zanzibar Football Association), kwa hiyo Rufaa hii imefutwa. Matokeo ya mchezo huo yanabakia kama yalivyo kama kuna malalamiko zaidi yapelekwe ngazi husika.
Wako,
………………………….
BETRICE SHABANI MGAYA
KAIMU KATIBU – TRFA
N.B HII BARUA UNAVYOIONA HAIJULIKANI INAENDA KWA NANI
LAKINI HUYO NDIO KATIBU WA TRFA TANGA AMBAE PIA ANATAKA KUCHAGULIWA UCHAGUZI UJAO. HAYO NDIO MAJIBU YA RUFAA ILIYOKATWA NA AIR SHOOTING.
No comments:
Post a Comment