Kaka shaffih jana nimeona kuna mdau wa soka ametuma ujumbe anataka ukweli jinsi gani hao Sport walikuwa wanataka kupanga matokeo kati yao na Prison ukweli ni huu.
Katika kundi lao (Kundi C) kulikuwa na timu 5
Kundi C
1. African Sports
2. Segera FC
3. Lushoto Shooting
4. Small Prison
5. Air Shooting
Hapa, kila timu inacheza michezo mine(4) na ikawa kama ifuatavyo:-
Tarehe 24 Feb 12 Saa 8.00 mchana
African Sports Vs Small prison matokeo droo bila kufungana
Tarehe 24 Feb 12 Saa 10.00 jioni
Lushoto Shooting Vs Segera FC matokeo Lushoto Shooting alishinda 3 kwa 2
Tarehe 28 Feb 12 Saa 8.00 Mchana
Air shooting Vs Small Prison Matokeo Droo bila kufungana
Tarehe 28 Feb 12 Saa 10.00 Jioni
Lushoto Shooting Vs African Sport matokeo droo bila kufungana
Tarehe 03 Mar 12 Saa 8.00 mchana
Segera Vs Air Shooting matokeo Air Shootin ilishinda gori 4 kwa moja
Tarehe 03 Mar 12 Saa 10.00 jioni
Small prison Vs Lushoto Shooting Small Prison ilishinda gori moja kwa 0
Tarehe 06 Mar 12 saa 10.00 jioni
African Sport Vs Air Shooting Matokeo African Sport ilishinda gori 1 na Air Shooting 0 mechi ambayo African Sport ilichezesha wachezaji toka Zanziber mechi hiyo ilikua kwao ni muhimu kushinda ili isonge mbele.
Tarehe 08 Mar 12 saa 10.00 jioni
Air Shooting Vs Lushoto Shooting matokeo Air Shooting ilishinda gori 2 kwa 0
Tarehe 09 Mar 12 saa 10.00 jioni
Segera Vs Small Prison matokeo Small Prison ilishinda gori 5 kwa moja
Tarehe 11 Mar 12 saa 10.00 jioni
African Sport Vs Segera Matokeo African sports ilishinda gori 3 kwa bila mchezo ambao haukuisha kutokana na kwamba wachezaji wa Segera waliamua kujikusanya pamoja na kukaa chini ndani ya Uwanja kuanzia dakika ya 34 baada ya kuona hawatendewi haki mpaka dakika zilizobaki zikaisha hivyo African Sport wakapewa point 3 na magori matatu.
Hivyo kwa matokeo hayo inakua kama ifuatavyo:-
Small prison point 8 na magori ya kushinda 6 na kufungwa gori moja
African Sport point 8 na magori ya kushinda 5 na hawakufunga gori
Air Shooting point 7 na magori ya kushinda 6 na kufungwa mawili
Lushoto Shooting point 4
Segera point 0
KWA MTAZAMO HUO
1. Kaka Shaffih angalia timu zilizoanza kucheza mchezo wa kwanza ndizo zilikua za mwisho kumaliza mchezo.
2. Kaka Shaffih angalia kutokana na Ratiba hiyo African Sport mechi zake zote zilichezwa jioni tunajiuliza kwa nini?
MAZINGIRA YA KUPANGA MATOKEO NA KUIBEBA AFRICAN SPORT.
1. Mechi za mwisho kati ya Segera Vs Small prison iliyochezwa tarehe 09 Mar 12 Small prison ilishinda gori 5 kwa 0 hivyo ikawafanya kuongoza kundi. Wakati huohuo Air Shooting wamekata rufaa yao dhidi ya mechi ya Air Shooting Vs African Sport kufuatia kuchezesha mchezaji kinyume na taratibu kwa maana kwamba ikikubaliwa rufaa yao basi wao watakua na point kumi na kuongoza kundi.
2. Mechi ya mwisho kati ya African Sport na Segera mechi ambayo haikuisha ambayo inadaiwa kuwa Prison waliongea na wachezaji wa Segera kua wasikubali kufungwa na mechi hiyo ilikuwa ni muhimu kwa African Sport make ilihitaji ushindi wa gori zaidi ya 5 kwa bila ili ifanikiwe kusonga mbele.
Kaka Shaffih hapa ndipo kulikua na vituko
Kufikia dakika ya 34 African Sport wameshapata magori matatu na hayo magori bwana ni aibu tupu uonevu mtupu ndipo wachezaji wa Segera FC walikusanyika kati kati ya Uwanja wakakaa chini wakawa wanaendele kunywa maji marefarii waliwabembeleza lakini walikataa wakidai kuwa kama wanawatakia sport ushindi wachukue mpira wapeleke gori wao wenyewe basi ukapita muda refa akamaliza mchezo na kuwapa African Sport point 3 na magori matatu. Hiyo haitosho African Sport wakakata Rufaa kuwa Small Prison imepanga matokeo na wao small prison wakata rufaa pia kuwa wameoneo kwa kupanga matokeo.
Kamati ya Rufaa ilipokaa ikaona timu zote zinamakosa ya kupanga matokeo hivyo African Sport na Small Prison zikatolewa kwa kosa hilo la kupanga matokeo na Air Shooting rufaa yao kamati ikadai kuwa iko juu ya Uwezo wao matokeo yanabaki hivyo.
Kaka Shaffih ukitaka ushahidi jaribu kuwasiliana na Redio moja ya hapa Tanga iitwayo Brizz FM walitangaza rufaa hizo na pia mwambie huyo mudau akutumie hizo barua z rufaa za timu hizo kama anataka ukweli. Sasa tunajiuliza nani ni nani msindi.
Kaka shaffih nasikia tena African Sport tena wamekata rufaa nafuatilia nitakujibu
Huo ndo ukweli ulivyo hapa Tanga katika ligi hii ya vituko
Wako katika Soka Bahati
No comments:
Post a Comment