NAME | PIUS KISAMBALE | |
NATIONALITY | TANZANIA | |
DATE OF BIRTH | 21 DECEMBER 1987 | |
HEIGHT | 5’8’ INCHES | |
WEIGHT | 68KGs | |
POSITION | STRIKER | |
JERSEY | 11 | |
PREVIOUS CLUB | Polisi Dodoma, Prison FC, Simba SC Polisi FC (Rwanda), Goha FC (India), Moro Utd, Mtibwa Sugar, Ruvu JKT |
NAME | ATHUMAN IDD | |
NATIONALITY | TANZANIA | |
DATE OF BIRTH | 18 FEBRUARY 1988 | |
HEIGHT | ||
WEIGHT | ||
POSITION | MIDFILEDER | |
JERSEY | 18 | |
PREVIOUS CLUB | Polisi Dodoma, Simba SC |
Mkuu Shaffih.
ReplyDeleteHili swali limeniacha hoi, haiingii akilini eti chuji ana miaka 24 hawa wachezaji huwa hawakui jamani, hizi ni rekodi za kuingizwa kwenye gueness book of records kama mtu umri wake unaweza kusimama mpaka mdogo wake wa kuzaliwa akampita hiyo ni record jamani.Kumbukumbu zangu zinaniambia Athumani Idd alijiunga na Simba akitokea Polisi Dodoma mwaka 2004 kwa mwaka huo ambao yeye anasema ndio alikuwa amezaliwa ina maana mwaka 2004 wakati anajiunga na Simba alikuwa na miaka 15, sasa sijui amejiunga polisi dodoma akiwa na miaka mingapi.
Pius Kisambale ni kweli kabisa ni mdogo wake Athumani Idd kwamba nini kimetokea mpaka akampita kaka yake umri ni wana sayansi wanaoweza kuchunguza na wakatupa formula ambayo inaweza kutumika hapo, sina maana ya kuthihaki ama kusema vibaya lakini tofauti ya umri kati ya mdogo-Kaka (Kisambale) na kaka-mdogo (Chuji) tofauti yao ni miezi 2 kwa mujibu wa details ambazo wao wamezitoa.
Swali hili limenikumbusha kizaa zaa cha Nurdin Bakari na Serengeti boys,TFF wamepeleka umri tofauti wakati huo huo Simba walipeleka umri wao tofauti pasipo kujua za mwizi ni 40.
Tuna mifano mingi tukianza kuizungumza hapa tutapata majibu ya undani kwa nini timu ya Taifa pia haifanyi vema, sula la umri wa wachezaji wa kibongo ni BOMU ambalo likilipuka litakuwa janga la Taifa.
Mdau.
Mike.
TEH TEH TEH TEH TEH!!! nimecheka kikatuni kwai hii mimi naona kama tutatafuta umri ya wachezaji wetu wa kibongo mmmmm nafikiri itakuwa kichekesho sana kwani hata kama utauliza swali kama hilo mwaka 2020 utaambia kwamba wote wana umri kati ya miaka 20 maana ni hatari mkuu
ReplyDeleteInawezekana mtu asijue kusoma lakini hata kuona picha tu iwe shida? Kwa kweli hili la kisambele na Kaka yake Chuji naona hata TFF wanalilea pia kwani si wana records jamani? Mimi nadhani Chuji yuko kwenye 30's. Pia ashitakiwe kwa kutoa details za uongo.
ReplyDeleteMimi nazani shida ni mfumo wetu wakitanzania wengi wetu hatuzaliwi Hospital
ReplyDeletetunazaliwa tukiwa majumbani kwetu,tutapatawapi vyeti vya kuzaliwa?.Wengi wetu tuna pata vyeti tukiwa watu wazima,so tunavitengeneza vyeti kulingana njisi tutakavyo vitumia baadae.Tungekuwa wote tunazaliwa hospital na tunapata vyeti wakati tunazliwa hingekuwa ngum kudanganya umri.Lakini kama tunapata vyeti wakati tunataka kushiliki mashindano flani au kujiunga na jeshi bado itakuwa laisi sana kwetu kutengeneza vyeti na kuweka umri wa uongo kulingana na maitaji ya sehem husika.Na siyo kwenye soka tu ata majeshini au sehemu ambazo wanazingatia umri wa mtu kuajiriwa au kupata kazi!.
waacheni hawa jamaa madudu km haya yapo maeneo yote unayoyafaham.tukisema tufuatilie ishu ya watu kuwa na vyeti feki na kuwachukuliwa hatua wahusika,amini nawaambia kuna taasisi zitafungwa kabisa!mfano nenda kwenye jeshi la polisi,jwtz,mahospitali utakuta watu kibao wenye vyeti fyongo wengi wanatumia vyeti vya washkaji zao.
ReplyDeleteFirst time namuona chuji personal ilikiwa pale sinza fast-food enzi hizo then mawella na swahiba wake boban by then walidai kwa maximo kuwa wana 22 iweje Leo awe na 24?uwongo mwingine ndo unatafsiri namna Watz na clubs zetu tunavyoendesha mambo yetu kibabaishaji
ReplyDeleteNimefanya kaz na mdogo wao wa kike Moro,nadhan now atakuwa na 28 na huwa anamwamkia chuji,huyo dada ni mtoto wa mama yao mkubwa kabsa
ReplyDeleteMorgan, tafadhali ebu acha uongo, mama yo alikuwa na mdogo wake ambaye amefariki miaka 2 iliyopita (21/12/2009) sasa huyo mama mkubwa anatokea wapi? nawaomba wadau mambo mengine tuyaache maana hata Data za uhakika hatuna
ReplyDeleteACHA MAJUNGU SHAFIH ,HUJUI UNAWEZA KUMHARIBIA KAZI CHUZI, KUMBUKA CHUJI ANATEGEMEA MPIRA KUENDESHA MAISHA YAKE SO UNAPOPOST MAMBO KAMA HAYA KWENYE BLOGS SIO MPANGO , UNAWEZA KUWA UMEWEKA KWA UTANI LAKINI IKAWA NA NEGATIVE EFFECT KUBWA KWA CHUJI KATIKA MAISHA YAKE YA SOKA. KWAN CHUJI NDIO MWANASOKA WA KWANZA KUKATA UMRI! TUACHE POROJO ZISIZO NA MPANGO BWANA...
ReplyDelete