Kama shabiki wa Inter Milan nimekuwa nikidekezwa katika misimu miwili iliyopita. Hii haihusiani na chochote kuhusu kushinda treble katika msimu wa 2009-2010 au 2010 Club World Cup.
Ilikuwa inahusu zaidi kuwa na nafasi ya kumuangalia mchezaji wangu kipenzi aliyekuwa anaijua kazi yake na kuifanya kwa ufanisi zaidi.
Mchezaji ambaye aliletwa kama Spare kipindi Ibrahimovic alipouzwa Barcelona. Mchezaji ambaye wengi wanamuona kama mfungaji tu japokuwa alikuwa na assists 22 na magoli 53 katika misimu miwili akiwa Inter. Ni mchezaji ambaye anatakiwa kutajwa kipindi ambapo wanapojadiliwa wachezaji bora wa dunia.
Huyu ni Samuel Eto'o Fils - world class footballer.
Najihisi mjinga kwa sababu nilimchukulia poa Eto'o. Ni haraka kiasi gani nimesahau namna ambavyo alikaribia kuipa Inter kombe la Scuddetto kwa mara ya 6 mfululizo msimu uliopita.
Alipouzwa kwenda Anzhi kiangazi kilichopita, ingawa nilikuwa disappointed, nilifikiri kombinisheni yoyote kati ya Forlan, Pazzini, Milito na Zarate mbele yao, huku Sneijder akisogeza mashambulizi kutokea katika midfield, ingeweza kuziba pengo lake kabisa. Wakati matatizo makubwa yaliyotukumba msimu yamekuwa ya ulinzi zaidi, timu pia imekosa mshikamano, ubunifu na umaliziaji katika tatu ya mwisho ya uwanja.
Huku kila mwaka unapokuja watu hufikiri labda namba zake zitashuka , bado katika michezo 13 at Anzhi mwaka huu tayari ameshafunga magoli 8. Lakini Eto'o anafanya vingi zaidi ya kufunga magoli, na ule uwezo wake kuweza kucheza nafasi zaidi ya moja inamfanya awe na thamani kubwa zaidi. Mchezeshe mbele akiwa na stikers wengine atawachanganya mabeki kwa kasi yake na kuwapa nafasi wenzie kufunga, Mchezeshe mbele pake yake, atawapeleka puta mabeki na kasi na ujuzi wake ndani ya 18.
Pamoja na ubora wake wote huu, Samuel Eto'o amekuwa undervalued player (Hapewi heshima anayostahili), kwa mfano msimu uliopita, alipotezwa na promo kubwa inayowazunguka Messi, Ronaldo and Rooney. Mwaka uliopita alifunga magoli 37, assists 15 katika mechi 53. Hizi ni number ambazo zinaonyesha kiasi gani ana uwezo huku akicheza dhidi ya ukuta mgumu wa Sere A.
The Bottom line: Samuel Eto'o ni mchezaji ambaye ni underrated (hathaminiwi) na pia wala hapewi heshima anayostahili katika soka.
Usiniamini mimi labda muulize Shabiki halisi anayeingia uwanja wa San Siro kila mechi huku akiwa hamuoni Eto'o dimbani.
Shafii nakuunga mkono mia fil mia kuhusu Etoo, na kikubwa ni ile rangi yake, labda wazungu wanaogopa asije akawa kama Weah..eti hawataki mweusi mwingine kuwe mchezaji bora wa dunia...
ReplyDeleterm