Alisema kwa sasa mchezaji huyo anaendelea vyema na matibabu na atatibiwa kwa muda wa wiki moja huku wiki nyingine akianza mazoezi mepesi mepesi kabla ya kujiunga rasmi na wenzake.
"Mwinyi ni mchezaji pekee wa majeruhi kwa sasa katika kikosi cha Simba kinachojiandaa na mechi yake dhidi ya Toto hapo kesho," alisema Kapinga.
Kuumia huko kwa Kazimoto ni pigo kubwa kwa Simba inayojiandaa na mechi ya hatua ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya ES Setif itakayopigwa kati ya Machi 24 au 25 jijini Dar es Salaam.
Mbali ya mchezo huo Mwinyi pia ataikosa michezo ya kesho dhidi ya Toto African na ile ya Jumatano ijayo dhidi ya Polisi Dodoma pamoja na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar.
Ushirikiano wa Kazimoto, Shomari Kapombe, Patrick Mafisango na Haruna Moshi umeisaidia Simba kutengeneza safu bora ya kiungo iliyochangia kupatikana kwa mabao 30 waliofunga hadi sasa katika Ligi Kuu.
Wakati huohuo; Wapinzani wao kwenye Kombe la Shirikisho, ES Setif imefuzu kucheza robo fainali ya Kombe la Algeria na leo watacheza dhidi ya JS Saoura.
ES Setif 'Mwewe Mweusi', wanaongoza Ligi Kuu wa Algeria kwa pointi 40, walipata ushindi wao mwepesi dhidi US Tebessa kwa mabao yaliyofungwa na Djabou dakika ya 43, na penalti ya Benmoussa dakika ya 80.
Mshambuliaji Djabou akiuzungumzia mchezo wao dhidi ya Simba alisema nawatakiwa kila la heri wenzangu."Mechi dhidi ya timu ya Tanzania haitokuwa rahisi, lakini nina matumaini tutacheza vizuri na kufikia lengo letu la kufuzu kwa hatua ya pili."
No comments:
Post a Comment