Wikiendi yangu ilianza siku ya ijumaa,Kama kawaida nilikuwa kwenye harakati za Kufanya maandalizi ya kipindi cha sports extra huku nikifuatilia mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye ulimwengu wa michezo kwa ujumla.
Mwenzangu kwa siku hiyo Alex Luambano alikuja na kunipa taarifa zilizozagaa mjini ambazo hata hivyo tulichukulia kama habari za mjini zinavyozagaa ambazo hata hivyo tulizipuuzia.
Taarifa hiyo ilikuwa inahusu Mchezo uliokuwa unatarajiwa kuchezwa siku inayofuata yaani jumamosi Kati ya yanga na azam fc kwamba kuna habari zimeanza kusambaa mitaani kuwa mwamuzi wa Mchezo huo Israel nkongo amehongwa na viongozi wa azam ili awapendelee kwenye Mchezo dhidi ya yanga .
Hata hivyo tuliziona Kama hazina ukweli ndani Yake kwani tumekuwa tukisikia maneno Kama haya Mara nyingi na hakuna hata Mara Moja ambapo taarifa hizi zimewahi kuwa na uthibitisho wa aina yoyote ile.
Nyuma ya pazia viongozi wa klabu ya yanga waliwaaminisha wachezaji wao kuwa mwamuzi amechukua fedha za azam na walifanya hivyo kwa kuwatahadharisha mambo Fulani ili kuepuka kupewa adhabu ambazo zingewagharimu Kama vile kadi nyekundu nk.Wachezaji waliopewa maelekezo ya kujichunga ni Stefano Mwasika na Nadir Haroub Canavaro pamoja na nahodha shadrack Nsajigwa ambao waliambiwa wahakikishe kuwa hawafanyi zile 'late tacklings' ambazo zingemuweka refa kwenye mazingira mepesi ya kutoa kadi nyekundu.
Mchezaji Mwingine aliyeonywa ni Haruna Niyonzima ambaye Mara nyingi huwa anapenda kuwa protected na refa,Niyonzima Aliambiwa apunguze malalamishi kwa refa .
Ukiachilia mbalimbali hilo taarifa zilisambaa pia kwa mashabiki wa yanga ambao hadi kufikia wakati wa Mchezo walikuwa wamejawa na hasira huku wakiamini kuwa azam inaelekea kubebwa na mwamuzi.
Wikiendi yangu ikaendelea kwa Kufanya kipindi Kama ilivyo Ada na Baada ya hapo nilirudi Kwangu kujipumzisha.
1.Stephano Mwasika akimchapa konde mwamuzi Israel Mujuni ( kadi nyekundu haikutoka )
2. Nadir Haroub akizuiwa kwenda kumvamia mwamuzi huyo kadi nyekundu ilitoka ).
Siku ya jumamosi nilikuwa naungoja Mchezo wa yanga na azam kwa hamu sana .mazingira ya nje ya uwanja yalikuwa yameutengenezea ladha ya msisimko mkubwa ambao ulinivutia kwenda kuutazama.
Mchezo wenyewe sasa ulianza kwa kasi kubwa huku timu zote zikionekana kuukamia . Mwamuzi Naye kwa upande wake alionekana kidogo kuathirika na Yale yaliyokuwa yanazungumzwa juu Yake kabla ya mchezo japo kwa kadri ya uwezo wake alijitahidi kuumudu Mchezo mwanzoni.
Baada ya hapo matukio ya kawaida tu ndio yaliyotokea ambapo kiungo wa yanga haruna niyonzima alionyeshwa kadi ya njano Baada ya kuupiga Mpira wakati mwamuzi alipoamua ipigwe foul.
Dakika chache baadae haruna niyonzima alijikuta akitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu iliyotokana na kadi ya pili ya njano ambayo aliipata Baada ya kumuonyeshea mwamuzi ishara ya kutokukubaliana na maamuzi Yake . Hapa ndio balaa lilipoanza , yanga walichanganyikiwa na kuanza kumkimbiza refa , stefano Mwasika Alimpiga mwamuzi ngumi ya USO ambayo kila mtu uwanjani aliishuhudia na hadi sasa hakuna anayeelewa ilikuwaje mpaka Mwasika hakupewa kadi nyekundu hasa Baada ya mwamuzi kuonekana akimuita na kuongea Naye na kisha kumuacha bila ya kumchukulia hatua yoyote, nadir haroub canavaro Naye kwa upande wake alionyeshwa kadi nyekundu Baada ya kuanzisha vurugu .
Mchezo ulilazimika kusimama kwa muda wa Kama robo saa hivi huku mwamuzi Israel mujuni akiwa muhanga wa vurugu zilizoibuka uwanjani hapo.
Mchezo uliendelea na mwisho wa siku matokeo yalikuwa ushindi wa 3-1 kwa azam.
Siku iliyofuata kulikuwa na Mchezo Mwingine Kati ya simba na toto Africa ya mwanza. Kwa haraka ukiungalia Mchezo Kama huu unategemea kuwa kwa mazingira halisi ya Mchezo toto afrika hawana chance ya kushindana na simba.
Lakini ukitazama nyuma ya pazia ndio unapogundua michezo michafu inayoendelea kwenye ligi ya Tanzania.
Taarifa ambazo hazina uthibitisho zinasema kuwa kuelekea michezo dhidi ya simba klabu ya toto huwa inaahidiwa fedha na klabu wapinzani wa simba Hali inayowafanya wachezaji kuukamia Mchezo kwa uwezo wao wote. Kwa jinsi Mchezo wa jumapili kati ya simba na toto ulivyoisha hapo ndio unapoweza kugundua ukweli wa mambo.
Kabla ya Mchezo toto ilikuwa kwenye Hali ngumu ya kiuchumi na kwa sababu hii ilikuwa imepoteza michezo kadhaa na ilikuwa kwenye eneo la hatari ya kushuka daraja . Hata hivyo jumapili toto ilicharuka na kucheza soka la Hali ya juu kuliko siku zake zote na kwa sababu hiyo wakapata pointi Moja Baada ya sare ya bila kufungana. .
Baada ya haya yote turudi nyuma na kujiuliza juu ya mwelekeo wa soka letu. Haya matukio kimsingi yanatia Mchezo aibu . Aina ya uchochezi toka kwa viongozi ambao ulianza kabla ya Mchezo wa yanga na azam ni ukosefu wa Dira ya kimaendeleo.
Wachezaji wanapoaminishwa kuwa mwamuzi atafanya mambo fulani dhidi Yao kimsingi wanaondoka kwenye Hali ya Mchezo na ndio maana unaona wachezaji wa yanga walipogeuka na kuwa wehu na kuanza kumkimbiza mwamuzi.
Kwa wachezaji nao hasa Stephano Mwasika , nadir haroub cannavaro , nurdin bakari na haruna niyonzima wanapaswa kuwaomba radhi wanachama na mashabiki wa yanga kwa kitendo cha kuitia aibu jezi ya timu hiyo kwa vitendo vyao ya aibu .
Stefano mwasika husasan anapaswa kukutana na adhabu Kali ambayo Itamfanya ajutie kitendo chake cha kumpiga ngumi mwamuzi. Wote tunajua kuwa waamuzi hasa wa ligi ya Tanzania Wana mapungufu makubwa lakini hiyo sio sababu ya wachezaji kujichukulia sheria mikononi. Stefano Mwasika anapaswa kufanywa kuwa mfano kwa wachezaji wote wenye Tabia za kuwapiga waamuzi.
Vitendo Kama hivi vinavyotokea kwenye soka la Tanzania vinafanya mchezo wa soka kushuka hadi na kupoteza mvuto wake mbele ya wapenzi wa soka na hata wadhamini ambao siku zone wanapigiwa kelele kuingia kudhamini Mchezo hawawezi kupata moyo wa kuingia na kuwekeza kwenye mazingira Kama haya.
Hello Shaffih.
ReplyDeleteBinafsi naunga mkono hoja kwamba wachezaji hawa wachukuliwe hatua kali za kinidhamu si kwa sababu naichukia Yanga la hasha ila ni kwasababu kumpiga refa si kitendo cha kiungwana katika mpira wa miguu, mpira wa miguu sio restling ama uwanja wa ngumi.
Ila viongozi wetu wa vilabu wawe makini sana kwani kwa namna moja ama nyingine wanapandikiza mentality mbovu kwa wachezaji, unapowaambia wachezaji kwamba Timu pinzani leo itapendelewa tayari unakuwa umeharibu concentration nzima ya mchezaji na hakuna ambalo mwamuzi atalifanya likaonekana zuri tena kwa sababu ya ile imani kwamba huyu anatuminya inakuwa imetawala kichwani.
Pamoja na mapungufu ya refaree ila tayari ile hali ya inferiority kwa timu ya Yanga ilishakuwepo kwani rekodi yao kwa siku za karibuni wanapocheza na Azam sio nzuri na Yanga wamekuwa wakikaa kwa gemu karibu 3.
Ni vigumu ligi yetu kuwa bora tukiendeleza uhuni kwenye soka naamini TFF watachukua hatua kali kwa timu ya Yanga na wachezaji husika na kwa mwamuzi pia kama alivunja sheria 17 za soka.
Mdau.
Mike.
Kaka Shaffih,
ReplyDeleteHongera sanaa, makala nzuri sana. Najua kuna mashabiki na wananzi hawataangalia kwa undani makala hii, badala yake wataisoma kwa juu juu na kukuona kama umeongea ili kuidhalilisha timu au wachezaji fulani, lakini kimsingi hii ni changamoto kwa timu, wachezaji, mashabiki na wadau wa soka kwa maendeleo ya soka letu.
Penye ukweli lazima usemwe ili watu wajifunze.
Bebeto.
Kuna ishu nyingi za kudisscuss sio hili hebu toa waraka mzito kushauri TFF juu ya nini kifanyike ili soka letu lipae sio kushikia bango hili au na wewe umetumwa kama nkongo nyauu we
ReplyDeleteTatizo lako Shaffii upo kiushabiki sana. kwa kutumia undishi wako wa habari unapenda kupotosha umma na huku unajifanya unajua. na ndio maana watu wanakusubiri uje ukae upande wa Yanga. katika matukio yote yaliyopo hakuna hata moja ambalo umeona Yanga wako sawa. kila jambo Yanga wamekosea. kumbuka jana kwenye kipindi cha clouds TV! Mchezaji wa Omega Seme ulivyokuwa unamsema vibaya. mwenzako Abdul Mohamed anakuambia angalia tukio wewe umekomaa kuisema vibaya Yanga. Kumbuka Yanga imeshiriki kwa kiassi gani kuleta Uhuru wa nchi hii ambao unakufanya wewe upayuke tu bila bugudha yoyote kuipata. sasa kwa kuwa umezidi sawa sisi tumuachia mola ndio atakayejibu sala zetu. maana katika jambo hili umekuwa mstari wa mbele katika kulishikia Bango utadhani ilikuwa timu yako ya Simba. kwa kuwa tunakujua wazi na wenzako wote mnaopotosha Umma kwa kutumia Kalamu yako basi mola mwenyewe ndiye atakayetutetea sisi waja wake. matendo aliyoyafanya Refa wewe yooote unaona yako. kazi aliyofanya Tegete, Nsajigwa na wengineo wewe hujaiona. sijui kwa kuwa walivaa jezi za Yanga kwa hiyo macho yako hayaoni? Punguza unazi ndugu yangu. Clouds Radio na Tv watu wanavipenda lakini unataka kupandikiza mbegu mbaya kwa wazalendo wa Nchi hii. mbona swali la Abdul Mohamed kuhusu ushirikina wa Simba na Toto hukusema? unabakia kusema Toto wamepata ufadhili na kupewa Hela ili washinde! tuna wasiwasi na upeo wa uelewa wako katika tasnia hii ya uandishi wa Habari. isije kuwa ujanja ujanja wa kuongea ndio unajifanya mwandishi! ipo Haja ya kukujua kiundani! sio kusema suala la Tambaza nimesoma n.k Kwa kweli unaboa! hadi radha ya kipindi unaiondoa! jirekebishe kulinda heshima ya Radio na Tv inayokupa ugali! we umuoni Mbwiga anavyoheshimu kazi yake?! Anakiri hadharani yeye ni Simba kabisa, lakini anapokuwa kazini haleti akili mgando kama yako! ukweli unatia kichefu chefu! inabidi utengwe katika Jamii!
ReplyDeleteMechi ya Simba na Kiyovu iliyokuwa chini ya Usimamizi wa Ofisi yako na wewe ukiwa Mratibu ilisababisha viti na vurugu kubwa sana sana kiasi cha Serikali kutoa Tamko kali. wewe mbona hujatoa makala ndefu na kali yenye michoro na picha kama hii? wakati hali halisi ilikuwa wazi kama Juzi?
Katika dini wanakwambia Haki huwezi kuletewa kwenye sahani ! haki ina taratibu zake hadi kuipata! sasa taratibu ndio kama hizo! ziwe ni sawa au sio sawa lakini ndio taratibu!
we shaffih unapayuka sana unashabikia kufungiwa kwa mtu kama omega seme wakati kati ya watu waliosaidia kupunguza vurugu ni omega seme.Acha unazi wa kipuzi kwenye soka nyau wewe ishia zako huko
ReplyDelete