Manager wa Real Madrid Jose Mourinho ametajwa kama kocha anayelipwa mkwanja mrefu zaidi dunianikatika listi iliyotolewa na jarida France Football.
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea anapata €14.8 million kwa mwaka huku warithi wake wawili pale Stamford Bridge wapo pia kati top 10.
Carlo Ancelotti anashika nafasi ya pili akiwa kocha wa PSG, akiingiza €13.5 kwa mwaka huku Guus Hiddink akishika nafasi ya tano katika listi akikamata €8.6m kwa mwaka akiwa na klabu ya Anzhi Makhachkala.
Barcelona wamekuwa na mafanikio makubwa sana hivi karibuni, lakini kocha wao Pep Guardiola halipwi vizuri kama Mourinho, akishika nafasi ya 3 kwa kulipwa €9.5m kwa mwaka.
Pamoja na timuyake kutokufanya vizuri katika ligi kuu ya Uingereza, Arsenal Wenger ndio kocha anayelipwa mkwanja mrefu kuliko wote kwenye EPL, akilipwa €9m kwa mwaka.
Boss wa matajiri wa Etihad, Roberto Mancini sasa anajitahidi kuweza kumfikia mpinzani wake Sir Alex Ferguson wa Man United, yupo nyuma ya Fergie, akiwa analipwa €5.9m kwa mwaka huku babu wa Scotland akiingiza €8m.
MOURINHO TOPS RICH LIST | |
Jose Mourinho (Real Madrid) Carlo Ancelotti (PSG) Pep Guardiola (Barcelona) Arsene Wenger (Arsenal) Guus Hiddink (Anzhi) Fabio Capello (Ex-England) Sir Alex Ferguson (Man Utd) Dick Advocaat (Russia) Jose Camacho (China) Roberto Mancini (Man City) | €14.8m €13.5m €9.5m €9m €8.6m €8.5m €8m €7m €6.1m €5.9m |
No comments:
Post a Comment