Search This Blog

Friday, March 30, 2012

MILOVAN: SIMBA TUNAENDA ALGERIA KUCHEZA KWA KUSHAMBULIA

Kocha wa Simba, Milovan Cirkovic, amesema hana mpango wa kucheza mchezo wa kulinda lango katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya ES Setif itakayochezwa kati ya Aprili 5, 6 na 7 mjini Setif, Algeria.
Simba itakipiga na wapinzani wao hao katika hatua ya 16 Bora ya kombe hilo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wikiendi iliyopita.
Milovan amesema kuwa ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mechi hiyo ya marudiano kutokana na uimara wa kikosi chake lakini anachotaka ni kuhakikisha wanafunga bao moja la mapema ili kuwavuruga wapinzani wao hao.
Kocha huyo raia wa Serbia, alisema mechi hiyo ya marudiano itakuwa ngumu kwao lakini watapambana dakika zote ili wapate bao moja na kusonga mbele.
“Tutakwenda Algeria tukiwa tunataka ushindi wa bao moja tu, ambalo tukilipata ninaamini tutasonga mbele katika michuano hiyo ya kimataifa.
“Hilo litawezekana kabisa, nina washambuliaji wenye uwezo mzuri wa kufunga kama Sunzu (Felix), Okwi (Emmanuel) na Boban (Haruna Moshi),” alisema Milovan.

No comments:

Post a Comment