DC Motema Pembe, klabu inayobebwa na mshambuliaji wa Kitanzania, Mussa Hassan Mgosi hivi sasa ndio inaongoza Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Timu hiyo ya mfungaji bora wa zamani wa Ligi Kuu hadi jana ilikuwa imekwishacheza mechi tatu, kushinda mbili na sare moja hivyo ina pointi saba.
Katika mechi ya kwanza, DCMP iliifunga Elima 2-0 ugenini na mechi ya pili iliifunga Saint-Luc 3-1 kabla ya kutoa sare ya bila kufungana na Makiso Jumatano.
Wababe hao wa Simba katika Kombe la Shirikisho mwaka jana, kesho wanashuka tena dimbani kumenyana na Muungano.
Timu nyingine katika Ligi Kuu ya DRC yenye washambuliaji wawili chipukizi wa Kitanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu na Mbwana Ally Samatta, Tout Puissant Mazembe inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake sita, ingawa yenyewe imecheza mechi mbili tu.
Mechi ya kwanza ilishinda 5-0 dhidi ya Tshinkunku na ya pili 1-0 dhidi ya Sanga Balende, wakati leo inamenyana na Molunge.
Machi 22, TP Mazembe itaanza kampeni zake za kuwania taji la tano la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kumenyana na Power Dynamos ya Zimbabwe mechi ya kwanza wakicheza ugenini kabla ya kurudiana nyumbani Lubumbashi wiki mbili baadaye.
Source:Bongostaz.blogspot.com
No comments:
Post a Comment