Timu zilivyoanza.
Athletic walianza mchezo kwa kasi kubwa na waliendelea na mchezo huo mpaka mwisho hali iliyowapa matokeo ya kuongoza ambayo wanarudi nayo mpaka Bilbao.
Sir Alex Fergusson aliamua kuwaacha bench Rio Ferdinand , Paul Scholes na Michael Carrick , Danny Welbeck huku akiwaanzisha Javier Hernandez na Wayne Rooney mbele na Chris Smalling na Johny Evans wakicheza kama mabeki wa kati.
Kwa upande wa Athletic , Marcelo Bielsa aliwachezesha wachezaji wake wale wale wa kikosi cha kwanza cha siku zote isipokuwa mchezaji Fernando Amorabieta ambaye alikuwa ana adhabu na nafasi yake ikachukuliwa na Mikel San Jose alianza kwenye nafasi yake . Athletic walikuwa timu bora tangu mchezo ulivyoanza wakishambulia kwa kasi huku wakimiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi.
Mifumo.
Bielsa kama tunavyomfahamu , anapenda kuchezesha timu ambayo nyuma anabakia mtu mmoja.Kama united wangechezesha mfumo wa 4-4-2 ya moja kwa moja basi Bielsa naye angechezesha wachezaji watatu kwenye defence yake badala ya kuchezesha mtu mmoja , lakini United walicheza na mfumo wa 4-4-1-1 na Bielsa alimpa Ander Iturraspe maelekezo ya kumkaba Wayne Rooney huku mtu mmoja akibakia kama mlinzi wa ziada hasa pale ilipotokea hali ya 1 v 1 dhidi ya Javier Hernandez.
Mfumo wa United ulikuwa mwepesi kwa Athletico kuukabili kwa kuwa walimtumia Ashley Young kulia , Ji sung park kushoto , wote hawa ni wachezaji wanaopenda kucheza kushoto lakini kwa kuwa jinsi Ashley Young anavyocheza inategemea kudrible mpira athari inayotokana na uwezo inategemea sana na upande wa uwanja anaocheza hivyo ingekuwa bora kama wangebadilisha winga park akaenda kulia na young akaenda kushoto. Park hata hivyo ni mzuri kwenye ulinzi na beki wa Athletic Andoni Iraola ni mzuri sana ilibidi Park acheze upande wake
Ukabaji
Athletic walikuwa wepesi sana katika mchezo wao huku wakiwa wanabadilishana nafasi mara kwa mara na walipokuwa hawana mpira walikuwa wanafanya pressing ya hali ya juu tangu upande wa mbele walipokuwa washambuliaji. Fernando Llorente alielekezwa kuwakaba mabeki wa kati huku wachezaji wa Athletic wa pembeni wakimsaidia Llorente na kufanya iwe hali ya 2v2 na badala ya kuwaelekea mabeki wa pembeni wa United ambao hawakuweza kupanda mbele bila bugudha ya wachezaji hawa.
Kama ilivyokuwa kwenye mchezo wao dhidi ya Barcelona , Atheltic walikuwa wanawakaba wapinzani wao man to man kila kona ya uwanja nah ii ilimaanisha kuwa Andre Herera na Oscar De marcos walipanda mbele kupindisha mianya ya kina Phil Jones na Ryan Giggs huku wakicheza mbele ya Iturraspe. Mara nyingi kulikuwa na shimo kubwa mbele ya Iturraspe na japo United hawakuwa na mtu ambaye angeweza kushambulia eneo hili , walipaswa kuwa na movement kwenye wingi zote mbili toka kwa Young na Park , wangeweza kukabwa lakini hii ingemaanisha kuwa wakabaji wao wangeacha nafasi huko wanakotoka na hatari ingeendelea kuwepo.
Mfumo wa ukabaji wa Athletico.Athletic Bilbao hawakuwapa United muda wa kupumua . Llorente alikuwa akikabana na watu wawili ili kubakiza mtu wa ziada mwisho wa uwanja , lakini hata hivyo mawinga waliwakaba mabeki wa pembeni , viungo wa kati walikuwa wakiwakaba viungo wa kati wa United na mabeki wa pembeni walikuwa wakiwakaba mawinga .
Upande wa nyuma mabeki walipokezana kumkaba Javier Hernandez japo Javi Martinez alifanya hivi kuliko wenzie na mshambuliaji huyu toka Mexico alipata tabu na watu waliokuwa wakimganda na beki aliyebakia alikuwa akicheza kama Libero.
Mashambuzli ya Athletic
Kitu ambacho Athletic walikifanya kwa ufasaha ni pale walipokuwa na mpira kwenye mashambulizi. Walikuwa wakiuhamisha mpira toka kwenye eneo moja hadi lingine kwa kasi kubwa huku wakicheza kwa uvumilivu wa hali ya juu pale waliponya’nganywa. Ufanisi kwenye mchezo wao ulikuja pale ambapo walipokuwa wanabadilisha kasi yao wakati walipokaribia eneo la hatari .
Mabeki wa pembeni walikuwa muhimu sana kwenye mchezo wa Athletic kwa kuwa walikuwa wakisambaza mpira kwa kutanua uwanja huku wakipanda na kushuka. Mara nyingi walikuwa wakipanda mbele sana karibu na goli la United na kuwa sehemu ya ushambuliaji na hakuna yoyote kati ya Park na Young aliyetaka kuwafuata na kuwakaba . Kwenye goli la kwanza la Athletico Iraola na Aurtenexte waliingia kwenye box la United na waliwazidi idadi wachezaji wa United na kumtengenezea nafasi Llorente.
Pasi
Jinsi pasi za Athletic zilivyokuwa zinapigwa hazikuwa na ufanisi sana lakini zilikuwa na malengo hasa ya kushambulia kwani ni kama wachezaji wa Athletic walitambua kuwa endapo watapoteza mipira wangewahi kuupata tena.
Kulikuwa na kitu cha kufurahisha kuhusu mipira mirefu . Bielsa aliwaonya Athletic kutocheza mipira mirefu iliyomuelekea Llorente tangu mwanzo wa msimu lakini bado wachezaji wa Athletic waliendelea kucheza mipira mirefu ya moja kwa moja iliyoelekezwa kwa Llorente huku mawinga wakihangaika kuwapita mabeki kupiga krosi .
Llorente alifanya kazi nzuri ya kukaa na mipira palie alipoipata kumngoja Llorente na viungo wa kati waingie eneo la hatari na kungoja krosi. Mabeki wa United kina Evans na Smalling bado hawajajenga ufanisi wa kucheza dhidi ya washambuliaji wenye maumbo makubwa .
Kosa walilofanya United ni kusimama eneo la mbele sana la uwanja mbali na lango lao wenyewe. Athletic waliwaelekeza washambuliaji wao kukaba lakini Rooney kwa upande wake hakuwa anafanya kitu alipokuwa hana mpira akimuacha Ituraspe adictate tempo ya mchezo na kuelekeza mipira pembeni mwa uwanja . Alielekezwa kufanya kazi kubwa kwenye kipindi cha pili wakati United wanafanya mabadiliko kwenye eneo la kiungo na kujaribu kuongeza nguvu na movement ya mpira .
Phil jones na Ryan Giggs walipata tabu sana , Jones hakuwa comfortable alipokuwa akipata mpira wakati mpinzani akiwa karibu yake . Giggs alikosa uwezo wa kukimbia maeneo mbalimbali ya uwanja na alipata tabu pale alipokabwa . Michael Carrick na Anderson waliingia kwenye eneo hilo na japo Carrick alifanya vizuri na kutengemaza midfield ya United .
Mwisho.
United walijua cha kutegemea toka kwa Athletic , lakini hawakujiandaa kwa aina ya mchezo wa kukaba toka kwa Athletic . Kiungo kilikosa movement na ufanisi pale wakati United ilipomiliki mpira . Hakukuwa na rotation ya nafasi na movement kwa ujumla haikuwa nzuri toka kwa United. Hernandez kwa upande wake hakuwa mzuri na alipoteza nafasi nyingi sana .
Huu pengine unaweza kuwa mchezo bora kwa Athletic kuliko yote waliyocheza msimu huu nah ii inatokana na mawazo ya kocha wao Marcelo Bielsa .
No comments:
Post a Comment