Wakala wa Dimitar Berbato amethibitisha kwamba mshambuliaji huyo anajiandaa kuondoka Manchester United dirisha lijalo la usajili.
Mbulgaria huyo ambaye alimaliza msimu uliopita akiongoza kwa ufungaji, amekuwa akihangaika kupata nafasi katika kikosi cha kwanza msimu akishindana na washambuliaji walio katika form Javier Hernandez na Danny Welbeck.
Hivyo wakala wa mshambuliaji huyo mwenye miaka 31, Emil Danchev sasa amekiri kwamba Boss wa mashetani wekundu amekubali kumuachia Berbatov aondoke mwishoni mwa msimu huu.
“Nimekutana mara tatu na Sir Alex Ferguson. Ni dhahiri inabidi tukubali kwamba Fergie atajaribu kujenga timu upya katika kipindi miaka kadhaa ijayo na kwa bahati mbaya Berbatov hayupo katika mipango yake.
“Nimefurahishwa na jinsi United wanavyolishughulia suala la mteja wangu, kwa kuwa wameweka wazi kwamba hawatoweka kizuizi cha namna yoyote katika kipindi cha uhamisho.”
Pamoja na Berbatov kuwa na umri mkubwa lakini meneja wake anasema mchezaji amemwambia hataki kucheza katika ligi ambazo hazina ushindani.
No comments:
Post a Comment