Search This Blog

Thursday, March 29, 2012

KALOU: VILLAS-BOAS ALINITISHIA SITOCHEZA TENA CHELSEA KAMA SITOSAINI MKATABA MPYA

Salomon Kalou alionywa na Andre Villas-Boas kwamba hatocheza tena katika kikosi cha Chelsea tena kama asipokubali kusaini mkataba mpya.
Mshambuliaji huyo alitoboa siri jana: "Niliambiwa na kocha aliyepita kwamba sitoruhusiwa kucheza mpaka nitakaposaini mkataba mpya.

"Labda alikuwa anajenga timu mpya na kufikiri kwamba sikuwa kwenye mipango yake ya baadae.

"Hii kitu ilinisumbua sana na iliufanya msimu huu kuwa mgumu mno kwangu kwa kutokupewa nafasi kabisa.
"Siku zote nimekuwa nikijituma sana na kuonyesha  kwamba hakukuwa na sababu yoyote itakayonifanya nisiwepo kwenye timu. Hii haihusu kuhusu pesa ni muda wa kuichezea timu yangu.

"Kama hupati nafasi ya kucheza, inakuwa ngumu sana na muda mwingine klabu inakuwa hainipi nafasi ya kuonyesha nini naweza kufanya  kwa ajili ya klabu yangu."

Kalou atamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu, alicheza mechi nne tu chini ya AVB.

Lakini ameshacheza mechi tano chini ya uongozi wa Roberto Di Matteo na kufunga goli pekee katika mechi ya champions league dhidi ya Benfica.                                                                                                 

No comments:

Post a Comment