Search This Blog

Sunday, March 11, 2012

DIDIER DROGBA AANZA MIPANGO YA UJENZI WA HOSPITAL KWAO IVORY COAST.

Mfuko wa Didier Drogba, leo utafanya hafla ya uchangishaji fedha katika hoteli ya Dorchester Hotel mjini London, lengo likiwa ni kukusanya kiasi cha pauni Milioni 3 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali nchini kwao Ivory Coast.
Zoezi hilo la tatu kufanyika katikia mradi huo, linatarajiwa kuhusisha watu kibao maarufu, wakiwemo wanasoka nyota duniani na wanasiasa, alisema mshambuliaji wa Chelsea.
  Vitu kibao, zikiwemo jezi za mchezaji huyo, rafiki zake na wachezaji wenzake, viatu, soksi na kadhalika vitauzwa kwenye zoezi hilo la hisani.
“Sapoti ambayo foundation yangu imepata hadi sasa ni babu kubwa, lakini bado tuna kazi zaidi ya kufanya,” alisema Nahodha huyo wa Ivory Coast.
Kituo cha afya cha Gigantic kinajengwa katika wilaya ya Attecoube mjini Abidjan, eneo la watu fukara ambalo linakosa hadi zana za kisasa za tiba.
Drogba alisema tiba na huduma kwa ujumla katika hospitali hilo, zitakuwa zikitolewa bure.
Mfuko huo (Didier Drogba Foundation) ulianzishwa mwaka 2007, kwa lengo la kushughulika na masuala ya kiafya na elimu Afrika.

No comments:

Post a Comment