Tottenham au Arsenal timu mojawapo inaweza kukosa nafasi ya kushiriki Champions league ikiwa Chelsea watashinda kombe hilo msimu mjini Munich – hata kama The Blues watamaliza katika nafasi ya tano msimu huu katika EPL.
`Chelsea wapo nyuma ya mahasimu wa London kusini katika Barclays Premier League na bado wana nafasi ya kuweza kumaliza ndani ya Top 4 ikiwa watafanya vizuri katika mechi zilizobaki.
Ikiwa watafeli kufanya hivyo, Europa league ndio mkombozi wao msimu ujao, kitu ambacho kinatafsirika kama kufeli kwa kiasi kikubwa kwa mipango ya mmiliki Roman Abramovich.
Lakini kama Chelsea wataweza kubeba taji la Champions league mjini Munich, May 19 watachukua nafasi ya mshindi wan ne wa EPL, katika timu zitakazoiwakilisha England katika Champions league msimu ujao, hata kama wakishika nafasi ya mwisho katika ligi.
UEFA hawataki kurudia mambo yaliyotokea 2006 wakati Liverpool waliposhinda Champions league na huku wakimaliza nafasi ya tano nyuma ya mahasimu wao Everton – na hatimaye timu zote tano za juu zilizruhusiwa kuiwakilisha England.
Msemaji wa UEFA akiongea na jarida la The People alisisistiza, kutakuwa na timu nne tu zitakazoiwakilisha England katika msimu wa 2012-13
“Ikitokea Chelsea wakachukua champions league na Arsenal wakamaliza wanne kwenye ligi, Gunners wataenda kucheza Europa ligi na kuwapisha Chelsea.”
No comments:
Post a Comment