Arsene Wenger yupo tayari kupambana na Chelsea kwa ajili kumsaini Eden Hazard.
Winga wa Lille ameshaangaliwa akicheza zaidi ya mara ya 20.
Lakini sasa Arsenal Boss Wenger amejitokeza na kusema hadharani kuwa anavutiwa mno na kinda hilo la Ubelgiji.
Wenger alisema: “Nampenda Eden ten asana, na kwa sababu nyingi sana.
“Uwezo wake wa kuuchezea mpira, kipaji chake cha kuweza kuwapangua wapinzani, muono wake wa mchezo, na kikubwa zaidi ni namna anavyoweza kupiga pasi za mwisho na ndio maana amekuwa akivigonganisha sana vilabu vikubwa.
“Hazard ana kila kitu cha kuweza kuichezea klabu kubwa, na Arsenal ni klabu kubwa.”
Wakati huo huo Arsenal wataenda Afrika na Mashariki ya Mbali katika kipindi cha kujiandaa na msimu mpya wa 2012-2013.
No comments:
Post a Comment