Rio Ferdinand amejitoa katika mbio za watu wanaotajwa kuweza kumbadili John Terry kama Naohdha wa England.
John Terry alivuliwa kitambaa cha unahodha leo asubuhi ikiwa ni mara ya pili katika maisha ya soka.
Rio Ferdinand ndiye aliyekuwa mrithi wa Terry mara ya kwanza alipovuliwa unahodha, lakini Manchester United defender amesema hataki hata kufukiriwa katika watu wanaopaswa kuchukua jukumu hilo la unahodha safari hii.
“Sitaki kuwa nahodha wa England baada ya yaliyotokea kipindi kilichopita,” Ferdinand alisema katika ukurasa wake wa Twitter.
“(I) Nataka kuweka umakini wangu katika kuichezea United na ikiwa nitachaguliwa katika kikosi cha England nitakuwa mwenye furaha.”
Na katika interview fupi iliyorushwa na BBC Rio alikaririwa akisema: “Nimeshakuwa nahodha wa England hapo nyuma kwa kipindi kifupi. Nilinyang’anywa kitambaa cha unahodha na kwa sasa nataka ni-concentrate katika kuitumikia United, kiukweli . Napenda sana kuichezea vizuri Manchester United.”
Ferdinand alikuwa aiongoze England katika kombe la dunia 2010 lakini akapata maumivu ya goti yaliyomuweka nje ya michuano hiyo
Ferdinand alikasirishwa na jinsi alivyotendewa na Capello wakati unahidha aliporudishiwa Terry mwaka mmoja uliopita huku mlinzi huyo wa United akiwa hajataarifiwa kuwa ameporwa unahodha huo.
No comments:
Post a Comment