Search This Blog

Tuesday, February 7, 2012

PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG: TUNDA LA MICHUANO YA MATAIFA YA AFRIKA 2012


Anaweza akawa amekosa penati ambayo imeigharimu timu yake ya Gabon kuikosa nusu fainali , lakini Pierre-Emerick Aubameyang ameibuka kuwa star wa michuano ya mataifa huru ya Afrika.

The 22-year old winger amefanya mambo makubwa katika michuano ya mwaka huu, na karibia aipeleke Gabon katika nusu fainali ya kihistoria ya African cup of Nations.

Alifunga katika kila mechi za makundi – akifunga katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Tunisia – na akitoa assists mbili, moja kwa Daniel Cousin katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Morocco na nyingine kwa Eric Mouloungui katika droo ya 1-1 dhidi ya Mali, droo ambayo Seydou Keita wa Barca alifunga goli la ushindi kwa Mali.

Aubameyang alikuwa ndio moyo wa mashambulizi ya Gabon katika michuano hii, na ndio alikuwa key player kwa “The Panthers”.

Muda mchache kabla ya michuano kuanza, Aubameyang alikamilisha uhamisho wa kudumu kutoka AC Milan kwenda AS Saint-Etienne ya Ufaransa.

Akiwa amejiunga na Milan in January 2007, mchezaji huyu wa zamani wa kikosi cha Ufaransa under 21 sio mgeni katika ligi ya Ufaransa, ameshacheza Dijon FCO, Lille OSC, AS Monaco na Saint-Etienne.

Baada ya kushindwa kupata nafasi katika Rossoneri first team, Aubameyang alienda kwa mkopo Les Verts mwanzoni mwa msimu wa 2011-12 kabla ya kuhamia moja kwa moja muda mchache kabla ya African Cup Of Nations kuanza.

Na kuna vitu viwili vitakavyokuwa vikiwasumbua AC Milan baada ya uhamisho huu.

Kwanza, ni vipi wamemuachia mchezaji ambaye ameibuka na kuwa hatari huku akiwa na umri mdogo.

Pili, ni vipi walikubali kumuuza kwa pesa ndogo inayofikia €1.8 million?

Hata kabla hajaenda katika African Cup of Nations na Gabon, tayari ilikuwa wazi kwamba kijana huyu ana potential ya kuwa mchezaji mzuri siku za mbele.

Kabla ya AFCON, alianza katika mechi zote 19 za ligi kwa klabu yake, akifunga magoli 6 na kutoa assists 4.

Pia alishinda “Man of the Match” awards na kutoa key passeskwa wastani wa 1.2 kwa mchezo.

Aubameyang alikuwa anaonyesha signs zote kwamba ataimarika na kuwa na uwezo mkubwa.

Kwa wale wanaongalia mechi za ligi ya Ufaransa wanaujua uwezo wa kinda hili na potential aliyonayo.

Lakini hata wale ambao ni washabiki wa dhati wa Ligue 1 wasingeweza kutabiri kwamba Aubameyang angekuwa na impact kubwa katika michuano hiiya AFCON, tena ukizingatia timu yake ya Gabon haikuwa inapewa nafasi kubwa ikishika nafasi ya 91 katika rank ya FIFA, na nafasi ya 20 in Africa kabla ya kuanza kwa AFCON.

Katika michuano hii, iliyoandaliwa na Gabon pamoja na Equatorial Guinea, versatile winger alionyesha uwezo wake wote wa kushambulia, akiwa na kasi, nguvu na pamoja ushahihi wa kutoa pasi ndani ya mchezo.

Katika michezo yote aliyocheza alikuwa akiwapeleka puta mno mabeki wa upinzani, na skills alizonazo alifanya kila awezalokuisadia Gabon kufika pale ilipoishia.

Kama ushahidi goli lake dhidi ya Morocco, Aubameyang anajua aupige vipi mpira na uende wapi katika net.

Na sio tu katika kushambulia ndipo uwezo wake ulipo, pia Aubameyang anajua jinsi kukaba ambapo hutumia kasi yake kuwa track washambuliaji wa wapinzani na kufanya successful tackles.

Msimu huu akiwa Saint-Etienne amefanikiwa kufanya tackles zilizofanikiwa 28 na kufanya interceptions 18.

Overall, mchezaji huyu ana kipaji sana na ana potential kubwa sana kuwa mchezaji mkubwa in future.

Ama kwa hakika AC Milan wakufikiri vizuri wakati wanaamua kumuachia kinda hili aondoke tena kwa fedha kidogo sana, angeweza kuwasaidia hata kushinda Serie A au UEFA Champions league titles.


1 comment:

  1. Tunapenda makala zako, lakini ni vema ukaamua kutumia lugha moja, kama kiswahili, basi kiwe kiswahili, na kama kiingereza basi kiwe kiingereza, kwa sababu ujue kuwa unawahudumia watu wenye uelewa tofauti wa lugha.

    ReplyDelete