Kocha mkuu wa Yanga, Kostadin Papic amemtaka kiungo Haruna Niyonzima kuripoti kambini mapema tayari kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo.
Niyonzima bado hajaripoti kambi ya timu hiyo, huku uongozi wa Yanga ukisema kuwa anatarajia kujiunga Alhamisi wiki hii.
Papic amesema mechi dhidi ya Zamalek siyo ya mchezo na hivyo anawataka wachezaji wote kuhakikisha wanajitahidia kwenye mazoezi ili waweze kushinda.Kuna uwezekano mkubwa mchezaji huyo kujiunga na wenzake siku hiyo ya Alhamisi ambayo timu hiyo itakuwa ikiondoka kwenda nchini Misri.
"Nina wasiwasi sana na Niyonzima, yeye ni miongoni mwa wachezaji muhimu kwenye kikosi. Namtegemea kwenye kikosi, lakini mpaka sasa sijamuona," alisema.
Lakini msemaji wa Yanga Luis Sendeu alisema Niyonzima anatarajia kujiunga na wenzake Alhamisi.
Niyonzima yupo Rwanda na kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa kucheza mechi kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.
Niyonzima yupo Rwanda na kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa kucheza mechi kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.
No comments:
Post a Comment