Search This Blog

Monday, February 27, 2012

MDAU WA BLOG HII ATUTUPIA LAWAMA SISI WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA SAKATA LA MBWANA SAMATTA!

Shaffih .
Kwanza kabisa heshima kwako mkuu, na nipongeze mabadiliko uliyoyafanya katika blog yako.

Kuhusu suala la Mbwana Samatta labda niseme tu kwamba mimi pia nilishangazwa sana niliposikia kikosi hicho bila kuwepo jina la Samata na lawama zangu za kwanza nilizipeleka kwenu waandishi wa habari ambao mlikuwepo ukumbini pindi kikosi hichi kilipokuwa kinatangazwa kwani mlipaswa kutusaidia kumbana kocha atoe sababu za kueleweka na sio kutuletea maneno yake ya ajabu ajabu.
Sina maana kwamba Samatta ni suluhisho la matatizo yetu kwenye timu ya Taifa ila hakuna asiyeujua mchango wa Samatta uwanjani hata kama hafungi goli ila timu inakuwa na uhai.Mimi binafsi sababu alizozitoa huyo mzee kuhusu kumuacha Samatta haziniingii akilini hata kidogo. Nina muheshimu sana huyo Mzee kwani ni kocha mwenye CV nzito na pia ni mkufunzi lakini hayo yote hayaaaminishi kwamba kwenye soka yeye anajua kila kitu, tumeona mifano mingi ya machocha bora kabisa wanakalishwa kitimoto pamoja na ubora wao itakuwa huyu Babu.
Angalia tukio lililotokea majuzi wakati Chelsea wanacheza na Napoli,AVB aliwaweka benchi Lampard,Essien na Cole ambaye alikuja kuingia baadae ya Bosingwa kuumia na timu ilipofanya vibaya Mmiliki wa Timu alimwambia AVB atoe maelezo ni kwanini aliwaweka benchi.
Suala la kuwa na viongozi wasiojiamini huleta matatizo kama haya ambapo wanaogopa kumuuliza kocha na kumbana mimi sina imani kabisa na watendaji wa TFF:
Huu sio muda wa kuleta mzaha na timu ya Taifa wakae wakijua tumechoka kuwa wasindikizaji wakati wao wanashibisha matumbo yao na huyo mzee akae akijua hatutaki utani hata kidogo tunataka matokeo sasa, masuala ya undumulakuwili hatuyataki tena.
Samatta bado ni mdogo sana na mchango wake unahitajika sana kwenye National team yeyekama anaona kijana hana uzalendo amuite kwenye National team kisha wakae wazungumze, mchezaji kutofunga kwenye mechi 2 za National team hakumaanishi hana uzalendo ndio maana Timu huwa zinakuwa na wataalamu wa Saikolojia ili kuwaweka wachezaji sawa.
Babu aache utani muda wa kutaniana umekwisha sasa ni matokeo.
Na hii TFF hii yaani basi tu

4 comments:

  1. Stewart Hall alishawahi kuwaambia waandishi wa habari kuwa, kutofunga kwa Ngassa katika mechi za Azam c sababu ya yeye kumuweka bench kwa kuwa uwepo wake uwanjani unatengeneza nafasi kwa wengine kufunga.
    Hivyo hivyo kwa Samata hata kama afungi uwepo wake unatengeneza nafasi kwa wengine na kupunguza ukali wa mashambulizi ya wapinzani

    ReplyDelete
  2. hayo mambo yenu ya kuingilia kazi za makocha ndio yanayo fanya soka linakuwa limejaa siasa. Mapenzi yako kwa Samatta hayamaanishi kwamba lazima awepo kwenye timu ya taifa. Kocha amefanya unyambulisho wake ameona Samatta hatasaidia timu, tayari kila mtu kishakuwa kocha tayari anataka kupinga maamuzi ya kocha!! Eti viongozi wa TFF hawajiamini wanatakiwa wambane kocha!! huo ulimwengu wa soka wa zamani kabisa. Kama humuamini kocha kuhusu maamuzi ya kumuacha mchezajji mmoja tu kwa nini unampa timu afundishe? acheni mambo yenu haya ya ushabiki usio na maana! Tumeamua yeye ndie kocha let him be our coach!! mpeni muda atekeleze program zako ambazo amepanga kutekeleza.

    Shabikia timu yako, nenda uwanjani kaangalie mpira kwa tiketi halali, nunua jezi, toa mawazo yako muda wa kuajiri kocha ukifika,toa motisha..haya mambo ya ukocha muachieni kocha. Ntakuelewa zaidi kama utaandika kuwa huna imani na uwezo wa kocha kwa ujumla,sio unasema una heshimu CV ya kocha ila TFF inabidi wambane anapofanya maamuzi kumuacha mchezaji usiye mpenda.

    A team needs one coach and one coach only!!

    ReplyDelete
  3. Kwanza nawapongeza wote, mtoa mada na wachangiaji..
    Mwanzoni nilikuwa napatwa na wasi wasi na nilitaka kumuuliza Shaffih kama TFF angalau wanapitia na kusoma Glob yake, lakini jibu nimelipata hapa. Mpendwa rk (iliyetangulia kucomment hapo juu)naamini kutokana na comment yako kwa njia moja au nyengine wewe ni mdau wa Soka na upo karibu na TFF, hivi umeona wapi kocha anapomuacha mchezaji ambae wadau/wananchi wanaamini na anaonekana hasa kutokana mchango na uwezo wake kwenye klabu wadau/wananchi wakakaa kimya? Umesahau sakata la Romario na Edmundo Brazil? Juzi tu hapa mashabiki na wanachama wa Ajax walikuja juu kwa uongozi wa Ajax ambao walipuuza mpango endelevu wa kuokoa club wa Mtaalam wa ufundi Johan Cruyff, hali iliyopelekea Bodi ya Wasimamizi (Board of supervisors) ya Ajax kujiuzulu, au hujasikia?. Itakuwaje wadau wasihoji kwa kitendo cha kumuacha Samatta ambacho ni sawa na kurejesha nyuma maendeleo ya soka hata kama ni kijana mmoja?.
    Napatwa na wasi wsi sana unapohimiza kukata tiketi halali na kununua jezi, bado tunarudi kuwa ndio wale waleeee wanaowaza mapato ya viingilio na mauzo ya jezi tu,mpenzi wa timu hahimizwi kukunua tiketi wala jezi, na wala mdau bora hahimizi watu kununua jezi na tiketi. Shabiki/mpenzi/mwanachama siku zote anaamini timu yake ni bora ndio maana anakuwa tayari kununua jezi na kulipia kiingilio bila ya kuhimizwa kwa ajili ya kuisapoti. Kiongozi bora wa soka ni yule anae karibisha maoni hasa kwenye sehemu ya ufundi, then yeye ataangalia yapi ya kuyafanyia kazi na sio kuhimiza kununua tiketi na jezi.
    Hata kama Samatta hana mapenzi na taifa lake kama ilivyosemwa, ingekuwa vyema kumuweka chini na kumuweka sawa kisaikolojia. Pia ingekuwepo option ya kumuita kambini akajifunza kwa wenzake. Samatta bado ni kijana mdogo ambae anaweza kulitumikia taifa kwa muda mrefu hapo baadae, haipaswi kumtelekeza na kumkatisha tamaa. Kama juhudi za kuongea nae hazitafanyika, kunauwezekano mkubwa wa kuathirika kisaikolojia kutokana na hili.
    Kama alivyosema Shaffih, kocha ana uhuru wake na sisi hatumuingilii ila tunapaswa kuhoji na kupatiwa sababu za msingi kwanini kijana kama Samatta anaachwa il-hali wanafanya vizuri sana kwenye klabu yake tena klabu kubwa kwa Afrika?!
    Iwapo Samatta unasoma comment hizi basi lichukulie suala hili kuwa ni changamoto ya kukuchonga ukali na sio issue ya kukufanya ukate tamaa, Watanzania tunaimani na wewe na bado tunakuhitaji.

    Mungu Ibariki Tanzania.

    Bebeto.

    ReplyDelete
  4. Bebeto,umetoa maelezo mazuri sana kama kuna watanzania ambao hawajaelewa kama huyo aliyepita basi tuwaombee mungu wajitambue,bado watakuwa kwenye group lile la usimba,uyanga pamoja na ttf yao.masamaki

    ReplyDelete