Search This Blog

Thursday, February 23, 2012

MAMBO MATANO YANAYOWAFANANISHA FELIPE SCORALI NA ANDRE VILLAS-BOAS NDANI YA KLABU YA CHELSEA.


Luiz Felipe Scolari Andre Villas-Boas 

Unagundua matokeo hajakuwa katika hali nzuri kama manager wa Chelsea pale ambapo unapofananishwa na Luiz Felipe Scolari.
Hali hii sasa ndio inayoomkuta Andre Villas-Boas baada ya kuwa na mfululizo wa matokeo mabayahuku jana akifungwa 3-1 na Napoli na kupoteza matumaini ya kusonga mbele.
Miaka mitatu baada tangu mbrazil huyo afukuzwe at Stamford Bridge,  Blog hii inakuletea makala ya namna ya Villas-Boas na Scolari wanavyofanana na kupishana kwa rekodi zao ndani ya klabu hiyo ya Chelsea.


UBORA WA KIKOSI WALICHOKIKUTA
Tangu 2004 kila kikosi cha Chelsea kimekuwa imara kikiwa na wachezaji kama Petr  Cech golini, John Terry kwenye ukuta, Frank Lampard kwenye kiungo na Didier Drogba katika ushambuliaji.
Lakini Scolari alikuwa na bahati kwamba wachezaji hawa muhimu walikuwa katika kiwango cha juu kabisa cha maisha yao ya soka, tofauti na AVB ambaye amewakuta Lampard na Drogba wakiwa tayari wameshafikisha miaka 34.
Scolari pia alikuwa nabahati alikuta kikosi chenye uimara mkubwa. Ricardo Carvalho alikuwa nguzo imara akisaidiana na Terry wakati Micheal Ballack na Florent Maloudawalikuwa watu wengine wa kiwango cha juu ndani ya safu ya kiungo.
Nicolas Anelka pia alikuwa kwenye peak hatari, na wenzake wakitengeza moja ya kikosi bora cha Chelsea katika miak ya karibuni. Villas Boas hajawa na bahati sana, kikosi kilichoachwa na Carlo Ancellotti  kilikuwa hakina uimara mkubwa baada ya kuuzwa kwa baadhi ya wachezaji.


REKODI ZA MASHINDANO
Kufuatia matokeo mabaya katika premier league,Scolari alitimuliwa baada ya michezo 25 baada ya droo ya 0-0 dhidi ya Hull. Iliwaacha Chelsea katika nafasi ya nne na pointi 10 nyuma ya viongozi wa ligi Manchester United.
Kwa idadi hiyo sawa ya mechi , Villas-Boas amepata ameshinda mechi 2 kati ya 10za mwisho akiwa nyuma ya pointi zaidi ya 15 nyuma ya vinara Man City , huku wakiwa hawana hata uhakika wa kufuzu katika Champions league – performance mbovu kuliko manager yoyote katika utawala wa Abramovich.
Scolari na AVB wote wana rekodi sawakatika Champions league group stage wakiwa na pointi 11, lakini Scolari alitimuliwa kabla hajakutana na Juventus katika hatua ya 16 bora.
Katika makombe ya nyumbani, Scolari alipita kirrahisi katika FACup tofauti naAVB ambaye kikosi chake kilibanwa nyumbani na Birmingham katika raundi ya tano. Japokuwa mbrazil huyo alikutana kipigo cha kushtukiza katika Carling Cup dhidi ya Burnley katika raundi ya nne huku Villas-Boas akitolewa na Liverpool katika robo fainali.


UHAMISHO WA WACHEZAJI
Villas-Boas hawezi kabisa kulalamika kwamba hakuwa na fedha ya usajili. Mreno huyo alitumia kiasi cha zaidi na paundi million 80 akijaribu kuimarisha kikosi chake lakini mpaka sasa ni mchezaji mmoja tu aliyefanya vitu vya kueleweka Juan Mata aliyenunuliwa kwa paundi million 29.
Gary Cahil bado anahitaji muda kuzoea mchezo wa timu wakati Orial Romeu ameonyesha ahadi lakini bado hajawiva kwa EPL. Eomelu Lukaku mwenye thamani ya paundi million 18 anaonekana yupo mbali sana mpaka kufikia uwezo wa juu, wakati Raul Meireles amekuwa akichez a vizuri tangu alipojiunga na Blues akitokea kwa Liverpool.
AVB alirithi kikosi dhaifu, lakini ametumia fedha nyingi kwa wachezaji ambao hawakuwa tayari badala ya kusajili quality players ambao wangetoa msaada mkubwa msimu huu. Kufanya mambo kuwa mabaya zaidi wachezaji wenye experience zaidi Alex na Anelka waliuzwa pasipo sababu ya msingi mwezi January.
Scolari alikuwa hakurupuki, lakini alikosea pale alipoanza kuleta ushkaji katika usajili baada ya kuwasaini wachezaji wake aliokuwa akiwaffundisha katika timu ya taifa ya Ureno, Jose Bosingwa, Deco ambao walitoa mchango mkubwa katika timu lakini akapotea maboya alimposaini Ricardo Quaresma  ambaye ali flop.
Scolari aliuza wachezaji kama Wayne Bridge, Shaun Wright Phillips, Tal Ben Haim,Khalid Boulahrouz, Steve Sidwell na Hernan Crespo. Wachezaji hawa wote hawakuwa na pengo ndani ya Chelsea cha zaidi alimsaidia Abramovich kupunguza matumizi.

 
SAPOTI YA MASHABIKI
Kulikuwa na mategemeo makubwa kwa Scolari ambaye aliitoa England katika mashindano ya kimataifa  mara tatu mfululizo akiwa na Brazil na Ureno, katika kufanya hivyo alionyesha  mchezo mzuri wa kuvutia.
 Bahati mbaya hakuweza kuifanya Chelsea icheze vizuri akitaka kuondoa mfumo wa Jose Mourinho, alianza vizuri lakini akafeli.
Kufungwa 1-0 dhidi ya Liverpool  at Stamford Bridge in October 2008 ilimaliza rekodi ya kucheza michezo 86 bila kufungwa nyumbani na mwezi mmoja baadae wakafungwa tena na Arsenal 2-1 pale darajani.
Mpaka kufikia mambo yakaanza kwenda kombo na mashabiki wakaanza kupoteza imani huku timu ikiendelea kupata matokeo mabaya. Miezi minne baadae timu ilikuwa ikizomewa dhidi ya Hull City na mabango ya mashabiki wenye hasira yalikuwa yameandikwa “Scolari Ondoka” na mashabiki walipata walichotaka baada ya mechi hiyo.
 
Pamoja na kuwa mtoto wa nyumbani ambaye alikuwa akimsaidia Mourinho wakati yupo Chelsea, uwezo wake mkubwa wa kujua kufundisha, lakini uzoefu wake mdogo wa kufundisha klabu kubwa kama Chelsea ndio unamwangusha AVB.
Kiuhalisia tu baada ya Chelsea kuwa na msimu mbaya kama ilivyo sasa, ni wazi kutakuwa na mashabiki wengi ambao tayari wameshakosa imani nae,ingawa wapo wanaosema mreno huyo apewe muda zaidi ili kuzoea. Anaweza kuwa na msimu mbaya kuliko Scolari lakini mwisho wa siku mpaka sasa kuna wazomeaji tu huku kukiwa hakuna mabango yakumtaka aondoke.


SAPOTI YA WACHEZAJI
“Pindi Scolari alipoanzakutoalawama kwa mchezaji mmoja mmoja hapo ndipo mambo yalipokuwa mabaya zaidi.” Haya ni maneno ya Drogba muda mfupi baada ya Scolari kutimuliwa, lakini hakuwa Didier tu aliyeleta mgawanyiko  katika dressing room, JohnTerry nae alikuwepo.
Wachezaji walikuwa hawana furaha na aina ya management ya Scolari ambayo ilionekana kumrudia. Lampard aliwahi kukaririwa kwamba wakati wa mwisho wa utawala wa mbrazili huyo wachezaji walikuwa hisia za kuweza kushinda kila wiki.
AVB nae alikuja na sera yake “my way or highway” pia imeonekana kuwa matokeo mabaya. Kabla yakuondoka kwa Alex na Anelka walifungiwa kuhudhuria ama kujihusisha na kikosi cha kwanza kwa mwezi  mmoja na morali ya timu iliaaanza kushuka tangu wakati huyo.
Mafaza wa Chelsea kama Lampard na Cole pamoja na Essien walipinga mbinu za AVB na jana wakawekwa benchi dhdi ya Naples, wakati kikao kilichoendeshwa na Drogba mbele ya camera za TV wakati wa mapumziko ya mechi dhidi ya Birmingham imezua hali ya maswali kwamba ndio mwamba na ana-run the show @Stamford Bridge.

No comments:

Post a Comment