Search This Blog

Monday, February 6, 2012

LIGI KUUYA ENGLAND NA MATOKEO YA KUSHANGAZA MSIMU HUU - MABEKI WAMEZIDIWA UBORA NA WASHAMBULIAJI?




Kwanza kabisa sielewi kwanini Jose Mourinho anataka kurejea England. Sidhani kama atafurahia mambo yalivyo hivi sasa katika soka la kiingereza.
Back in 2004, kipindi cha msimu wake wa kwanza in EPL, Mourinho alishangazwa sana na habari kutoka White Hart Lane ambapo matokeo ya mahasimu wa North London kati ya Tottenham Hotspur na Arsenal yalikuwa 4-5.
“Haya sio matokeo ya soka,” alisema Mourinho, “Haya ni matokeo ya Hockey. Muda mwingine mazoezini , tunacheza mechi, watatu dhidi ya watatu, na matokeo yakiwa 5-4, nawarudisha wachezaji vyumbani. Kama wanashindwa kuzuia vizuri, kwanini tujisumbue?
Imagine Mourinho angekuwepo England kipindi hiki ambapo kuna matokeo ya Man United 1-6 City, Man United 8-2 Arsenal, Chelsea 3-5 Arsenal.
Tottenham Hotspur 1-5 Man City. Manchester City 3-2 Tottenham 2.
Na sasa hili jana Chelsea 3-3 Manchester United. Tena Chelsea wakitangulia mbele kwa goli 3 – 0, then wanakuja kurudishiwa magoli yote katika dakika 26 za mchezo.
Kama Mourinho alishangazwa na kuudhiwa na matokeo ya mechi yaliyojumlisha magoli 9, angesemaje katika hali kama hii ya sasa, ambapo Chelsea moja ya timu alizozifundisha wanashindwa kulinda advantage ya kuwa mbele kwa 3-0?
Mashabiki wa Chelsea watajaribu kumlaumu mwamuzi Howard Webb, na penati mbili za kipindi cha pili, lakini atleast ya pili unaweza ukaiita ‘soft penati’, lakini inaweza ikawa kama malipo ya penati mbili walizonyimwa United katika kipindi cha kwanza.
Hakuna atakayebisha kwamba United walistahili kuipata draw. Walikuwa wanacheza vizuri kuliko Chelsea, hata ambapo walipokuwa nyuma kwa goli 3 hawakuonekana kukata tama walishambulia vizuri chini uongozi wa muingereza mwenye mapafu ya mbwa Wayne Rooney.
So nini kimetokea kwa mabeki wa premier league msimu huu? Inawezekana wamezidiwa ubora na washambuliaji hatari waliopo katika ligi hiyo.
Rooney, Sergio Aguero, Robin Van Persie, Fernando Torres, Luis Suarez, Demba Ba, na wengine kama Javier Hernandez, Adebayor, Dzeko, Drogba, na Jermain Defoe.

MATATIZO YA SAFU YA ULINZI YA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND.
Tatizo la ulinzi katika premier league pia ni jambo lingine litakalomtia matatizoni kocha wa England katika michuano ijayo ya EURO.
Akiwa amekaa katika directors’ box, Fabio Capello, jana alikuwa na hali furaha na huzuni kwa wakati mmoja. Kuona washambuliaji wake wakiwa kiwango cha juu, Wayne Rooney akionekana kuanza kurudi kwenye form huku Danny Wellbeck akizidi kuimarika, lakini pia aliona namna ya mabeki wake wa kati Gary Cahil na Rio Ferdinand wakishindwa kucheza vizuri kabisa.
Rio Ferdinand ni mchezaji kivuli ambaye kuna kipindi alikuwa ndio nguzo kuu ya ngome ya Manchester United lakini sasa anatia shaka. Akiwa anazomewa kipindi chote cha mechi na washabiki wa Chelsea, alionekana kituko mbele Fernando Torres.
Kwenye benchi alikaa nahodha aliyevuliwa kitambaa John Terry, akiwa majeruhi wa kimwili na kiakili.
Kwa mtazamo wa kisoka kutoka pale uwanjani, hakukuwa na kitu ambacho kingemfanya Capello aache kuwa na wasiwasi na kutokuwepo kwa John Terry katika kikosi chake.
Hamna lolote kutoka kwa Ferdinand liloonesha yupo karibu kurudi kiwango chake cha juu, kwa upande wa Gary Cahil  pia hakuonekana kama ana ubora wa kuongoza safu ya ulinzi wa kufanya combination kati yake na aidha Phil Jagielka, Joleon Lescott, Chris Smalling au Phil Jones.
Terry anaweza akawa mtu ambaye anaweza kuleta mgawanyiko ndani chumba cha kubadilishia nguo, lakini England hawana mchezaji mwingine ambaye ana sifa kama zake kwa sasa.
    

No comments:

Post a Comment