Ni zaidi ya miaka ishirini sasa, Waingereza wamekua na kiu ya kufanya
vizuri katika michuano ya kimataifa. Pamoja na kufanya vizuri sana
katika ngazi ya vilabu lakini hali ni tofauti kabisa kwa upande wa
timu ya taifa.
Tangu kuisha kwa zama za akina Paul Gascoigne 'GAZZA'
mwanzoni mwa miaka ya tisini, pamoja na kuwa na wachezaji wazuri kama
Michael Owen, Steven Gerrald, Frank Lampard na sasa Wayne Rooney bado
waingereza hawajaweza kata kiu yao.
Baada ya kushindwa kufuzu kucheza fainali za Euro 2008 chini ya Steve
McClaren, Waingereza waliamua kumpa mkataba 'mnono' muitaliano FABIO
CAPELLO, huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika
michuano ya kombe la dunia 2010 pale bondeni kwa mzee Madiba, mambo
yalienda mrama kabisa na simanzi ilitanda zaidi pale ambapo watani wao
wa jadi Ujerumani wakiwazamisha kwa jumla ya goli 4-1 na kuwatoa
mashindanoni, kwa upande wangu sikuwa na budi kusema kuwa Fabio Capello
alichangia kwa kiasi kikubwa kutofanya vizuri pale kwa Jacob Zuma.
Aina ya mpira aliokua anafundisha 'slow but sure' ilikua ni ngumu kwa
Gerald na Lampard 'wazee wa counter attack' huku timu ikiwa haina mtu
kama Pirlo au Seeldorf, pia Capello alishindwa kuwaamini 'young stars'
kama Joe Hart, badala yake akimtumia Robert Green 'pazia' eti azuie
mashuti ya London Donovan na Clint Dempsey, huku akimuacha Scott
Parker eti hana uwezo, mmh...! haingii akilini. Shaun wright Phillips
kwa Walcott? jibu mnalo.
Kuelekea Euro(2012) mwaka huu, kujiuzuru kwake nakuchukulia kama ni
kuogopa lawama na aibu kwani sidhani kama Capello angekata kiu ya
Waingereza zaidi ya kurudia machungu yaliyotokea pale kwa mzee
Madiba.
Skendo ya John Terry na kauli za Capello zilikua ni 'excuses'
kwa kitakachotokea Euro kama angekua 'incharge'. Kwa mtazamo wangu
Waingereza hawana cha kupoteza baada ya kuondokewa na Fabio Capello,
kwani hakupata funzo 'lesson' kutoka kwa Joachim Loew ambae aliwaamini
'madogo' akina Mesut, Muller, Khedira n.k huku Capello akimpigia simu
Rio Ferdinand eti anamhitaji Euro mwaka huu kanakwamba hawaoni
'madogo' kama Chriss Smalling, Walker, Micah, Cahil n.k
Mwisho kabisa naweza kusema kua Waingereza wanamhitaji kocha anaeujua vizuri mpira wa kiingereza, pia mwenye uwezo mkubwa wa kuwasaikoloji wachezaji.
By Simon Chimbo
Capello maji yalizidi unga, Ni wakati wa Harry Redknapp
ReplyDelete