Search This Blog

Tuesday, February 28, 2012

GARY NEVILLE: GIGGS NA SCHOLES WANAWAONYESHA WACHEZAJI WAKUBWA NAMNA YA KUCHEZA KWA MAFANIKIO UNAPOKUWA UZEENI.


Kitu cha kuvutia kimetokea katika kipindi cha miaka 10 ndani ya premier league. Wachezaji ambao walionekana ni watu ambao wasingeweza kupata nafasi katika vikosi vya kutafuta makombe kutokana na umri wao mkubwa sasa wamekuwa ndio muhimu zaidi katika timu zenye kutafuta mafanikio.

In fact, kikosi cha kinachofaa siku hizi kwa ajili ya premier league kinabidi kiwe kinawachezaji nan echini ya umri wa miaka 23, kumi na mbili walio kwenye umri wa miaka 23 na 33, na wanne au watano walio na umri mpaka wa miaka 38.

“Miaka 5 iliyopita ndani ya Manchester United, tulikuwa tukipewa presentation kuhusu maabara moja maarufu iliyopo at AC Milan, ambapo kutokana na sayansi nzuri ya michezo na lifestyle ya kiafya, wamefanikiwa kuwaweka wachezaji kwenye hali nzuri watakapoingia katika umri wa miaka 30 na kuendelea.

Kikosi cha AC Milan  kilichochukua kombe la ulaya kikiwa na wachezaji wenye umri mkubwa.in 2007
“Walituonyesha watu kama Alessandro Costacurta, ambaye katika kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 40, Cafu alikuwa na miaka 36, Serginho 35 na Paolo Maldini akiwa na miaka 38, na wote hawa walikuwa wakicheza. Lengo la United lilikuwa na kuwaweka sawa kiakili wachezaji kuendelea kucheza soka la ushindani watakapokuwa katika miaka ya 30.

Katika soka kuna vipindi muhimu sana kama viwili. Unapokuwa kijana – inaweza kuwa ndani au nje timu. Then kati ya umri wa miaka 21-30, then hapo unakuwa kama mfalme, moja ya nguzo katika kundi la wachezaji watano au 6 ambao huanza kila mechi.

Lakini kama utacheza kila Jumatano na jumamosi na kila mashindano kipindi cha kiangazi wakati wa umri wa miaka 21-30 . Ni lazima utakuja kudondoka kileleni utakapofikia umri wa miaka 32. Majeruhi yataanza kukuandama na kupona kwa haraka haitakuwa rahisi tena.

Unapofikia hatua hiyo kwanza vitu viwili vitatokea, utagundua mabadiliko ya kimwili na utaanza kujitunza vizuri zaidi, pili kiakili, utakubali kwamba huwezi tena kuwa tegemezi.
Nilikumbushwa hilo nilipokuwa Naples wiki iliyopita, nikiangalia Chelsea katika champions league ambapo manager Andre Villas-Boas alipowapiga benchi Micheal Essien, Frank Lampard na Ashley Cole.

Na pia nikiangalia na namna mambo yalivyo ndani ya klabu ile, huku story zikisema na  manager mwenyewe akikiri kwamba wachezaji wamekuwa wakim-challenged kuhusu maamuzi yake ya jinsi ya kupanga kikosi, hapo ndio napata majibu kwamba kuna wachezaji ndani ya Chelsea ambao bado hawajakubaliana na mabadiliko halisia yanayotokea kwenye career zao.

Cole na Lampard wana hali ngumu sasa ndani ya klabu yao.
Kwa sababu unaweza kuona kwa ushahidi wa kimwili, hawapo kama walivyokuwa miaka minne au mitano iliyopita. Lakini kama wangekubaliana na ukweli huo – na kama wangekuwa wanaongoza vizuri na manager wangewaeleza majukumu yao mapya na kuwafanya wao kama sehemu ya majukumu hayo – wangeweza kucheza at Chelsea mpaka watakapokuwa na miaka 37 au 38.

Mwangalie Jamie Carragher pale Liverpool. Watu wanaweza kusema ‘atakuwa anakasirika kuwekwa benchi akiwa na umri wa miaka 34.’ Lakini kiukweli anaweza Akakaa na ku-relax akiwaacha vijana wawili ambao wanacheza vizuri waendelee.

Atachangia pale atakapohitajika kwasababu lazima itafikia wakati utahijika. Kama utaweza kukubaliana na ukweli kwamba muda wako wa kuongoza vita ukiwa mstari mbele umekwisha, then unaweza ukarudi nyuma na kuwa jenerali wa vita hiyo. Ni wachezaji aina ya Carragher ambao watakuwa viongozi kwenye dressing room, wakisistiza nidhamu na kutoa ushauri na kutia moyo wachezaji wadogo pale inapohitajika.

Wachezaji wachanga wanatakamuongozo, na kama utaangalia wachezaji kama Juan Mata, Daniel Sturidge, David Luiz na Gary Cahil, sidhani kama wanapata muongozo.
Inaonekana kana kwamba kuna vita ya kuonyeshana umwamba zaidi ya hali ya AVB kukubali kwamba hawa wachezaji ni muhimu na wachezaji wenyewe kukubali kwamba majukumu yao yamebadilika kutoka na umri wao.

Mfano kwa wachezaji ni Ryan Giggs, akiwa tayari ameshacheza mechi za mashindano 900 katika level ya juu na sasa ana miaka 38.

Giggs na Scholes mifano ya kuigwa.
Usiku wa alhamisi iliyopita, camera ziliivuta sura yake baada ya Danny Welbeck akiingia uwanjani dhidi ya Ajax na ilikuwa wazi kabisa kwamba asingeweza kukamilisha idadi ya mechi 900 usiku huo. Alikuwa katulia, miguu ikiwa juu bila kujali akijiweka tayari kwa mechi dhidi ya Norwich. Hakukuwa na habari yoyote kuhus yeye kunung’unika kuhusu kutoswa kule katika mechi ile. 

Paul Scholes nae yupo na tabia kama za Giggs.

Kama utaiangaliwa Arsenal kipindi hiki ambapo hawajachukua makombe, ambacho kitakuwa ni miaka 7 mwishoni mwa msimu, unaweza ukasema kwamba Arsene Wenger aliwaondoa mapema wachezaji kama Patrick Vieira na Roberto Pires.

Na wachezaji wa aina ile katika dressing room na uwanjani tena kwenye mechi kubwa, timu zake zingekuwa zimekomaa kiakili kuliko sasa. Labda wasingeweza kutoa msaada mkubwa kihivyo lakini wangeweza kuleta tofauti.

Rio Fedinand ameanza kufikia hatua hiyo katika maisha yake ya soka, na labda umeanza kuona ishara hizo pia kwa Steven Gerrard, kwa majeruhi yaliyomkuta. Itamtokea Wayne Rooney pia katika miaka 5 au 6 ijayo lakini mchango wake utaendelea kuhitajika klabuni.

Kama una miaka 32 na unawekwa benchi, usipaniki  kuhusu suala hilo. Chill out, na tulia. Umeshapigana vita yako. Sasa nenda kapigane vita ambayo unahitajika kupigana.

Kwasababu nini ni njia mbadala kama utashindwa kukubali kwamba wewe sio tena top player wa kikos? Ni kwenda China au Russia kuichezea Anzhi?au kuishia katika timu za level ya kati katika premier league.?

Ni vizuri kuweza ku-manage mategemeo yako, kaa katika klabu kubwa na kuwa kiongozi mzuri kwa vijana walio ndani ya timu nab ado unaweza ukaendelea kushinda makombe kama Ryan Giggs na Paul Scholes.
  

No comments:

Post a Comment