Fulham wamemsaini mchezaji wa zamani wa Real Madrid kiungo Mahamadou Diarra mpaka mwishoni mwa msimu, wakiwa na option wa kuongeza mkataba mpaka mwishoni mwa msimu ujao.
Diarra mwenye umri wa miaka 30, ambaye ameshaichezea Mali mechi 74, atasaini mkataba pale atakapopata viza ya kufanyia kazi.
Kiungo huyo mzuiaji amekuwa mchezaji huru tangu alipoondoka Monaco kipindi cha kiangazi kilichopita baada ya timu hiyo kushuka daraja.
Diarra alianza career yake at OFI crete na Vitesse Arnhem, kabla ya kwenda kuunda ukuta wa kutisha katika safu ya kiungo ya Lyon pamoja na Micheal Essien.
Aliichezea Lyon mechi 172 na kushinda makombe 4 mfululizo ya ligue 1 kutoka 2003-06.
Alisajiliwa na Real Madrdi na Fabio Capello in 2006 kwa ada ya £22million na alikuwa mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi kilichoshinda La-liga in 2007 na 2008.
No comments:
Post a Comment