Search This Blog

Tuesday, February 21, 2012

EXCLUSIVE : FERGIE NITAENDELEA KUWEPO UNITED HATA NIKISTAAFU - MOURINHO ATAPATA UHURU MKUBWA OLD TRAFFORD.

 
Sir Alex Ferguson amesema ataendelea kuwepo Manchester United kipindi atakapoacha kazi ukocha.
Fergie anasema bado ana miaka miwili au mitatu ya kuendelea kukaa katika benchi la United na anaamini kutakuwa na kazi nyingine atapata ndani ya klabu hiyo pale atakapostaafu.

Mscotland huyo mwenye miaka 70 anasema  anaweza kuwa balozi wa klabu kama ambavyo Sir Bobby Charlton alivyo ndani ya klabu hiyo.
Similar role: Ferguson is keen to take a role at the club similar to that of Sir Bobby Charlton
Balozi wa Manchester United Bobby Charlton. Kazi anayoitaka Fergie baada ya kustaafu.


“Nitabaki hapa. Nafikiri kutakuwa na nafasi ya kazi ndani ya United kwa ajili yangu baada ya kumaliza kazi yangu ya ukocha,” aliiambia BBC Radio 5 katika mahojiano yaliyorushwa leo jioni.

Supportive dad: Sir Alex Ferguson takes advantage of a rare Saturday off to go and watch his son Darren's Peterborough side beat Bristol City 3-0 at London Road
Baba mwenye mapenzi: Fergie alienda London kumuangalia mwanae Darren Ferguson akikiongoza kikosi chake cha Petersbough kikishinda mechi dhidi ya Bristol City at London Road juzi jumamosi.

Katika wakati wake ndani ya United ameshinda makombe 12 ya premier league, mawili ya champions league,matano ya FA Cup,na manne ya Carling Cup na kuifanya United moja ya timu iliyofanikiwa zaidi barani ulaya na dunaini kwa ujumla.
Fergie mwanzoni alipanga kustaafu mwishoni mwa msimu wa 2001-02 baada ya United kushinda taji,lakini aliamua kuendelea kubaki United na kujenga kikosi kingine cha United kilichozidi kumpa mafanikio.
“Nafikiri kila siku watu wanapenda kuondoka wakiwa wamtoka kushinda,” anasema Ferguson.
“Natumaini nitafanya hivyo. Sijui kwa muda gani nitaendelea kuwepo lakini kama afya yangu itaniruhusu nitakuwepo Old Trafford kwa miaka mingine 2 au 3.”
Kitu kimoja kinachomfurahisha zaidi Fergie na kumpa muamko wa kuendelea na ukocha ni upinzani dhidi ya Liverpool ambao anasema haupo wala haujawahi kuonekana sehemu nyingine yoyote.
.
Best of Enemies: Ferguson thinks the rivalry with Liverpool is unparalleled
Maadui: Fergie anasema anapenda upinzani uliopo kati ya United na Liverpool.

Aliongeza: ‘Hiki kitu kuhusu sisi na Liverpool ni upinzani, tena wa wa hali ya juu. Kunakuwa na mechi  zenye ushindani wa hali ya juu ndani na nje ya uwanja. Ndio timu zenye historia kubwa katika soka la Uingereza kwa upande wa mafanikio na ndio maana hizi timu kila moja inamhitaji mwenzie.”

Kumekuwepo na maneno na tetesi kuhusu mtu atakayemrithi Ferguson huku wachezaji wa zamani wa klabu hiyo wakihusishwa na kazi hiyo kwa mara kadhaa.
Lakini Jose Mourinho anabakia favorite kwa kwa kutwaa nafasi ya ukocha at Old Trafford na Sir Alex Ferguson anaamini mreno huyo atapata uhuru mkubwa akiwa United kuliko anaoupata sasa akiwa na Real Madrid.

Ferguson  pia alizungumza kuhusu maisha yake nje ya soka,akikiri yeye ni “mteja” wa soka ambaye anatumia muda wake mwingi kuangalia soka wakiwa na wajukuu zake.
“Kwa kawaida naagalia mechi kila usiku. Kwa hali ilivyo siku hizi kwenye soka, kunakuwa na mechi katika kila usiku. Siku pekee ambayo labda unaweza ukakosa kuwepo mpira ni Alhamisi na sasa nitakuwa na nahusika na mechi za siku hiyo.’
Always delivers: Ferguson says his wife Cathy is keen for him to be a milkman when he retires
Fergie akiwa na usingizi wake Cathy, ambaye anataka mumewe awe muuza maziwa atakapostaafu.

Pia alimzungumzia mke wake  ambaye anasema huwa anamwambiaga akistaafu soka awe muuza maziwa  atakapostaafu kuifundisha Manchester United.
Fergie pia alikiri anamiliki Ipod na huwa anasikiliza muziki, “Nina nyimbo kama 15 katika Ipod: Sinatra, Nat King Cole, Patsy Cline, Willie Nelson na nyingine za namna hiyo.”

Ilipozungumziwa tabia yake ya kupenda wine, Ferguson alizungumzia kikao kimoja cha baada ya mechi na Sam Allardyce.
Good friends: Ferguson enjoys a day at Newbury races with West Ham manager Sam Allardyce
Fergie akiwa na rafiki yake kipenzi kocha wa West Ham Sam Allardyce.

“Big Sam aliniletea wine moja nzuri sana wakti tunaelekea kukutana uwanjani miaka mingi iliyopita wakati wa siku yangu ya kuzaliwa.
“Manager wa mtunza vifaa aliniletea asubuhi ikiwa imefungwa na karatasi, hivyo nikaifungua na kuibadilisha na chupa ya Ribena. Tulikutana baadae na akaniambia hii ni ya kwako utaifungua baadae lakini nikamwambia hapana nitaifungua hapa sasa hivi ili tunywe wote. Nilipoifungua ile chupa akakimbia na kumfuata mtunza vifaa huku akiongea kwa sauti kubwa. Nilidhani atamuua.”

No comments:

Post a Comment