Mchezaji star wa club ya soka ya AZAM FC beki Erasto Nyoni, amekiri kwamba club ya Azam imechangia kuyabadilisha maisha yake katika kipindi chote cha miaka minne toka ajiunge nayo.
Erasto mwenye umri wa miaka 29 akiwa ni baba wa mtoto mmoja, tayari mpaka sasa ametumia zaidi ya milioni 15 kwenye ujenzi wa nyumba yake Tabata hapahapa 88.4 Dar es salaam, nyumba ambayo ni matunda ya mshahara na posho za Azam na pia anatembea amekaa ndani ya Carina ya milioni 7 aiyoinunua mwaka jana.
Japo alifanya kazi za muda mfupi na club tofauti zisizo pungua tatu, Hicho ndicho kikubwa alichovuna Erasto nyoni toka amekuja Dar kwa mara ya kwanza mwaka 2001 akitokea 89.8 Singida ambapo alikua kumsalimia kaka yake, lakini baadae akaanza kucheza soka kwenye uwanja wa sifa Mtoni kwa Aziz Ally.
Baadae alipata kazi aliyoifanya kwa mwaka mmoja, kazi ya ujenzi huko Tabata kwenye kampuni moja iliyokua inamlipa elfu 90 kwa mwezi, pembeni na kazini kulikua na uwanja wa mpira wa Segerea Rangers kwa hiyo akawa akimaliza kazi saa kumi alafu akawa anaingia uwanjani kupiga mazoezi.
Wakati huo kulikua na timu ya ligi daraja la nne ya Segerea Rangers kocha alikua Sebastian Mkoma ambae yuko TFF kwa sasa ambae ndio alihusika kumtoa na kumtafutia nafasi katika klabu mbalimbali za soka ikiwemo ya AFC na nyingine ya Burundi ambapo alipokua huko ndio alipigiwa simu na kujiunga na Azam miaka minne iliyopita.
huyu jamaa anajua sana nakumbuka ndie aliyepiga bao kule Burkinabe wakati wa Maximo
ReplyDelete