Chama cha soka cha England kimeonywa juu ya sumu inayowezwa kusambazwa katika timu ya taifa ya England ikiwa John Terry ataitwa na kwenda katika michuano ya EURO 2012.
Terry anatuhumiwa kumtukana kwa kumtolea maneno ya kibaguzi Muingereza mwenzie Anton Ferdinand na kesi yake amabyo ilitajwa jana imepangwa kusikilizwa July 9, tarehe ambayo itakuwa baada ya kumalizika kwa michuano ya EURO.
Lakini Jason Roberts, mchezaji wa zamani wa Blackburn ambaye amehamia Reading na pia ni maarufu kama mchambuzi wa soka katika radio, anasema Terry hapaswi kuitwa na inabidi aondolewe katika kikosi cha England atleast mpaka kesi yake ya ubaguzi itakapoisha.
Pia anasisitiza hoja ya boss Fabio Capello kuwa Terry hapaswi kuhukumiwa kabla hajapatikana na hatia sio sahihi kwa kesi hii kwa sababu hata kaka yake Anton alitimuliwa katika kikosi cha ENGLAND kabla hajapatikana na hatia na FA kwa kukacha kupima vipimo vya matumizi ya madawa.
Akiwa katika mtandao wa Twitter, Roberts aliseama: “Nimeona kesi ya Ferdinand na Terry imesogezwa mbele. Siamini kama ni sahihi kwa nahodha wa England kwenda katika Euros.
“Msemo wa hakuna hukumu kabla ya kupatikana na hatia haufanyi kazi mara zote katika soka kama ilivyokuwa kwa Rio Ferdinand in 2003. Pia muhimu zaidi, naamini dressing room ya England at EUROS itakuwa imegawanyika na hiyo inaweza ikawa sumu.”
Situation ya Terry inaweza kuzungumziwa katika kikao kijacho FA.
Lakini inaeleweka Capello anataka kumchukua Terry kwenda nae EURO kama kiongozi wa timu.
Macho yote sasa yategeukia @Stamford Bridge jumapili hii ambapo Terry anakutana na Rio Ferdinand wa Manchester United kaka wa Anton.
The Premier League committee imesema utaratibu wa kupeana mikono utaendelea kama kawaida katika mechi hiyo – tofauti na walivyofanya FA katika mchezo wa Carling cup kati ya QPR na Chelsea.
No comments:
Post a Comment