John Terry amevuliwa unahodha wa timu ya Taifa ya England kwa mara pili katika maisha yake ya soka.
Terry aliitwa na leo saa 4 asubuhi na Mwenyekiti wa FA David Bernstein na kuambiwa uamuzi uliochukuliwa na bodi ya maamuzi ya FA.
Uamuzi huu FA utakuwa umemuudhi kocha Fabio Capello ambaye yeye siku zote amekuwa akimtetea Terry na aliweka wazi ndiye atakayekuwa nahodha wa England katika EURO 2012.
Pia FA imempa muda wa kufikiria Terry kama bado anataka kuiwakilisha timu yake ya taifa katika EURO, lakini wamesema hatolazimishwa kufanya maamuzi kwa haraka.
Waingereza wanajikosha,wameona kwamba njia waliyotumia kumuadhibu luis suarez haikua sahihi,kwanini kesi ya ubaguzi wa rangi ipelekwe polisi badala ya maamuzi kutolewa na chama cha soka? Na kwanini basi suarez nae asishtakiwe polisi? Wao wakakurupuka kumuadhibu kwa ushaidi dhaifu.
ReplyDelete