Search This Blog

Thursday, February 23, 2012

AHSANTE SANA KAMATI YA LYATOO KUUSIMAMISHA UCHAGUZI WA DRFA, SASA TUWAGEUKIE VIONGOZI WA TEFA MAANA HAWANA SIFA PIA..

Tafiti mbalimbali zinaonesha kwamba katika nchi nyingi duniani ambapo viongozi wa soka wameng’ang’ania madaraka kwa kipindi kirefu bila kuleta mabadiliko kiwango cha soka kimekuwa kikishuka.
Hali hiyo ndiyo inayojitokeza hapa nchini baada ya watu wachache kuhodhi madaraka hali inayowafanya Watanzania wanaotafuta maisha kupitia tasnia hiyo wakibakia masikini.
Kitendo hicho kimekuwa kikituchukiza sana sisi wapenda soka kwani ni ajabu kubwa sana tena sana kwani kwa hali hii ni ajabu kubwa kama kuna nchi zilizopiga hatua za kimaendeleo kwenye mchezo huu kutokana na vitendo kama hivi.
“Kiukweli hii ni moja ya sababu inayofanya soka letu lisiende kule tunapotarajia liende kutokana na watu wachache kung’ang’ania madaraka”.
Ukiwa kama mpenda soka la Tanzania utakuwa unafuatilia kwa umakini huu uchaguzi wa chama cha soka cha mkoa wa DSM yaani DRFA na jinsi baadhi ya viongozi wanavyong’ang’ania na kupigania kwa hali yeyote ile katiba isibadilike ili isiwatupe mkono miongoni mwao ambao hawana sifa.
Takwimu zinaonesha kwamba, kundi kubwa la viongozi wa chama hicho hawana sifa za kiungozi kulingana na katiba mpya itakayopitishwa hali inayonifanya mimi kutamani kulia kama sio kutamani kufa kabisa.
Lakini hapa ninachotaka kukizungumzia kiujumla ni kuhusiana na mtandao mkubwa sana ambao ukiuchunguza utagundua kuwa viongozi hao wanaowania nafasi hawana shida na soka wala mpira wenyewe bali wao wanashida na pesa na ndio wasichotaka kukiacha.
Kwa muda mrefu, DRFA wamekuwa na utaratibu wakuingilia chaguzi zote za wilaya tatu yaani Temeke, Ilala na Kinondoni  na kama hauko kwenye mtandao huu huwezi kushinda uchaguzi  wowote kwenye wilaya hizi tatu kama wewe si mwana mtandao na hilo halina ubishi watafute wadau wa Temeke wakujuze.
Hali hiyo pia imejitokeza wilaya za Kinondoni na Ilala, kwa undani zaidi si vibaya ukawauliza Abdallah Bulembo,  Frank Mchaki au refarii Mstaafu Abdukadir watakueleza kilichowakuta.
Mbali na hilo, wengine waliowahi kukutwa na suala hilo ni Mbunge wa Kinondoni ambaye ni mdau mkubwa wa michezo Iddi Azzan ambaye alikuwa haukubali uongozi wa DRFA  lakini naye akakubali matokeo na kunyoosha mikono juu na akapata nafasi ya kuwa kiongozi Kifa na baadaye DRFA.
Lakini cha kujiuliza hapa ni je, uongozi huu umekaa madarakani miaka mingapi? Hivi leo wanaweza kuieleza jamii mafaniko yao kwenye soka kwa ujumla hapa mkoani DSM.
Kama hilo linashindikana, pengine wangetueleza sababu za wao kukwama kisoka licha ya wao kukaa madarakani kwa kipindi kirefu bila tija yoyote.
Tumejionea badala ya viongozi wa DRFA kuandaa mechi za kirafiki ambazo zingekuwa zinakiingizia mapato chama hicho, wamekuwa wakisubiri mechi za Yanga na Simba ili kupata mapato kiduchu yasiyoweza kukiendeleza chama hicho na soka la Dar es Salaam kiujumla.
Kuonesha kwamba viongozi hao sio wabunifu, wasio na fikra za kimaendeleo kisoka, viongozi wa DRFA wamekuwa wakigawana mapato ya mechi palepale uwanjani mara baada ya mchezo kugawanyika.
Unaweza usiamini hali hii, lakini ninachokisema naomba ukipata fursa ukifanyie kazi na naamini utapata uwezo wa kuhoji nani anayeweza kutunza ama kudhibiti mapato na matumizi kutokana na mtindo wa kuwekana madarakani waliojiwekea.
Ndiyo maana hadi sasa huwezi kuwa kutoka Temeke, Ilala au Kinondoni ukaenda kulalamika kuhusu vyama hivi kwa jambo lolote kwa DRFA, utakuwa umejiingiza kwenye matatizo na uongozi wake.
CHAGUZI ZA WILAYA
Kama mtakumbuka hakuna uchaguzi uliokuwa na matatizo kama uchaguzi wa wilaya ya Temeke, nadhani sijawahi kuona uchaguzi wa vichekesho kama  ule kwenye maisha yangu yote ya kushabikia soka manake vichekesho vilianza toka pale rasimu ya katiba ilipokuwa inataka kupitishwa pale ukumbi wa Polisi Changombe yaliyopo Makao Makuu ya Wilaya ya Polisi Temeke.

Kwenye ile Katiba kulikuwa na kipengele kimoja ambacho leo kinaleta mtafaruku mkubwa DRFA ambacho ni elimu. Chenyewe kilikuwa kinasema, yeyote yule anaweza kugombea uongozi iwapo atakuwa na elimu inayofanana na kidato cha nne, je nyie wenzangu ni elimu ipi inayofanana na hiyo?
Nakumbuka ulikuwa mkutano wa vichekesho sana tena sana na ndio maana haukuisha vizuri. Licha ya baadaye kuambiwa fomu za uchaguzi zimeanza kutolewa lakini kuelekea mchakato wa uchaguzi uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa uchaguzi wa DRFA, MUHIDIN NDOLANGA watu wengi walikatwa ili wasishiriki kwenye uchaguzi huo.
Ukiachana na hayo, cha ajabu watu waliwakatia baadhi ya wagombea rufaa mfano Katibu wa Tefa wa sasa BAKILI MAKELE yeye ni Mwenyekiti wa serikali wa mtaa hapa kata ya 14 aligombea kama darasa la saba lakini tefa alikuwa kidato cha nne!
Sio huyu tu, bali Mwenyekiti wa Tefa ukiachana na sifa ya kutuhumiwa kutokuwa Raia, lakini alitumia cheti cha mtu kugombea uongozi katika wajumbe wa kamati ya utendaji.
Vile vile pia kuna huyu anayefahamika kama SAID AKIDA na Bwana STELEKI wote hawana elimu ya kidato cha nne tumgeukie Makamu Mwenyekiti Bwana RAMADHANI NDONGA yeye ndio anasoma QT sasa.
Lakini wote hawa, rufaa zao zilitupwa na wote walishinda bila ya kupingwa na kama kulikuwa na mpinzani basi alipandikizwa ili ionekane kuwa kulikuwa na mgombea. Kama ulikuwa hujui, hii ndio ilikuwa DRFA ‘Utake Usitake’ lazima ukubali.
Kwa hali kama hii, mimi na wewe tutumie fursa hii kujiuliza, kweli DRFA itaweza kuendeleza soka la Dar es Salaam kwa mtindo huu? Nawasilisha.

1 comment:

  1. Shaffih ndugu yangu kuna watu wapo Drfa toka mimi nasoma shule ya msingi miaka ya 80 mpaka hii leo sijui hawaoni haya?kwani hakuna tija yoyote mpaka leo,its me Yahya toka Dar maene6 ya Gerezani.

    ReplyDelete