Jack Wilshare anatarajiwa kukiongezea nguvu kikosi cha Arsenal mapema mwezi ujao.
Kiungo huyo wa kimataifa wa England amekosa nusu ya msimu wote kutokana na majeraha ya enka ambayo aliyapata katika michuano ya Emirates Cup.
Sasa timu ya madaktari wa Arsenal wanaamini kiungo huyo ataanza kufanya mazoezi na timu mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi ujao.
Mechi ya Barclays premier league dhidi ya Bolton on February 1, inaonekana itakuwa mapema sana kwa kiungo huyo kuweza kucheza, lakini kocha Arsene Wenger ana matumaini kumchezesha Wilshare katika mechi dhidi ya Blackburn tarehe 4 mwezi wa pili au mechi dhidi ya Sunderland siku saba baadae.
Ideally, Wenger anataka Wilshare apate match fitness kabla ya mechi ya Champions league dhidi ya AC Milan February 15.
Pamoja na maendeleo mazuri aliyonayo Wilshare madaktari wa Arsenal wamesema watamruhusu kiungo huyo arejee uwanjani pale tu watakapokuwa na uhakika wa 100% na si vinginevyo.
No comments:
Post a Comment