Search This Blog

Friday, January 20, 2012

WENGER: TUTASHINDA DHIDI YA UNITED


Manager wa Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa timu yake bado ni washindania ubingwa pamoja na kwamba kwa sasa wapo katika nafasi mbaya ambayo inaweza hata kuwakosesha nafasi ya Champions league.

The Gunners wanakutana na Manchester United wikiendi hii, klabu mbili ambazo katika miaka michache iliyopita ndio zilikuwa zikigombea utawala wa soka la England, lakini sasa wamekuwa wakipambana na upinzani wa Chelsea, Manchester City na Tottenham Hotspur katika kuutafuta ufalme wa soka England.

Ingawa, mbele ya mchezo wa Jumapili kati ya Gunners na United at the Emirates Stadium, Wenger amesema : “Hali ipo vilevile. Sio mchezo pekee kwa sababu kuna mchezo mwingine kati ya Chelsea na Man City unakuja, huku Liverpool wakiwa wanasubiri. Lakini mchezo kati yetu na United, ni mechi inayotazamwa dunia nzima.

Akiizungumzia mechi yao dhidi ya United ambayo siku ya jumapili inatazamiwa kujaza viungo wengi , lakini Wenger timu yake ina kila kitu kuweza kushinda mechi hiyo.

“Muda mwingine United wanakuwa wazuri sana katika kiungo na kufanikiwa kuua mchezo wetu wa pasi na kutuwahi katika counter attack. Wanafanya hivyo vizuri.

“Naamini kwamba inawasaidia sana, ingawa mwaka jana tuliwafunga 1-0 katika mchezo wa kuvutia zaidi. Inategemea ni jinsi gani tutacheza siku hiyo, tutacheza kwa pasi na kupitisha katika mistari yao, haijalishi watakuwa wengi kiasi gani.”

Wenger ana matumaini kuwa na mlinzi wake Thomas Vermaelen katika mechi hiyo, lakini Thierry Henry ana asilimia chache za kucheza mechi hiyo na kurudisha uhasama wake na Red Devils.

No comments:

Post a Comment