Wote kwa pamoja walikuwa na thamani ya £85 mwaka mmoja uliopita, lakini sasa Fernando Torres na Andy Carrol hawawezi kununua goli.
Washambuliaji hawa wamekuwa waki-struggle tangu walipovunja rekodi za uhamisho mwezi January last year na mambo hayakuwa mazuri pia kwao katika mechi za jana.
Torres, aliyenunuliwa kwa ada ya £50million ndio mchezaji ghali zaidi ndani ya EPL history, jana alistua kidogo kwa kugongesha mwamba kabla ya baadae kupewa kadi ya njano kwa kujirusha katika ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Sunderland.
Mbadala wa Torres at Anfield, Carroll aliyenunuliwa kwa £35million, aliachwa benchi na kocha Kenny Dalglish mpaka kipindi cha pili katika mechi iliyoisha 0-0 dhidi ya Stoke, mechi ambayo aliishia kujiangusha na kuwaacha mashabiki wa upinzani wakiimba “upotevu wa fedha”.
Torres na Carroll wote wamefunga mabao mawili kwa kila mmoja katika EPL msimu huu, na kwa kuwaongezea aibu hata veteran aliyestaafu na kurudi uwanjani akifunga bao katika mechi yake pili tu tangu apige U-turn na kurudi uwanjani.
No comments:
Post a Comment