Kiungo wa Manchester City Nigel De Jong yupo katika hatihati ya kuuzwa in the summer baada ya kukataa kusaini mkataba mpya @Etihad Stadium.
Dutch International De Jong alikuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa City lakini alikataa kusaini mkataba mpya wenye thamani ya £100,000 per week kipindi cha kiangazi kilichopita.
Sasa De Jong amejikuta nje ya mipango ya kocha Roberto Mancini na inaeleweka City watasikiliza ofa mwishoni mwa msimu ikiwa the 27-year old ataendelea na msimamo wa kukataa kusaini mkataba mpya.
De Jong anapendwa zaidi na mashabiki wa City lakini katika siku za hivi karibuni amekuwa akichoma mahindi benchi baada ya Mancini kuwa anawatumia zaidi Yaya Toure, Gareth Barry na James Milner.
City bado wameweka ofa mezani lakini mpaka sasa hawajasiliana tena na kambi ya De Jong.
Huku Mancini akiwa anatambua kuwa wachezaji wengine inabidi wauzwe kabla ya kufanya usajili wowote, De Jong anaweza akawa sacrificed ili kutengeneza nafasi ya kusajiliwa kwa viungo wengine. Hatouzwa katika dirisha hili dogo la usajili.
Lakini lolote linaweza likatokea, ikizingatiwa sasa japokuwa Yaya Toure hayupo na Owen Hargreaves akiwa hayupo fit, De Jong bado anakosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza katika mechi kadhaa zilizopita ikiwemo ya hivi karibuni dhdi ya Wigan.
No comments:
Post a Comment