Michuano ya Kombe la Mapinduzi inafikia tamati leo kwa timu ya soka ya Azam ya Dar es Salaam kumenyana na Jamhuri ya Pemba.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na msisimko na ushindani wa hali ya juu kutokana na timu zote hizo kuonyesha soka safi tangu mwanzoni mwa michuano hiyo.
Azam ilifika hatua ya fainali baada ya kuwachapa mabingwa watetezi, Simba, mabao 2-0
katika mechi ya nusu fainali huku Jamhuri ikiifunga Mafunzo ya Unguja mabao 2-1 katika mechi nyingine ya nusu fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Amaan juzi usiku.
Fainali hiyo ambayo itachezwa saa 2:00 usiku wa leo, inatarajiwa kushuhudiwa pia na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, ambaye ndiye mgeni rasmi katika siku muhimu ya kuadhimisha siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika mchezo huo wa juzi, Jamhuri ilicheza mchezo safi na wa kufundishwa kitu ambacho
kimeweza kumpa jeuri kocha wao, Renatus Mayunga ambaye ameahidi kuwa atatumia
uzoefu wake ili aweze kutwaa ubingwa huo.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa pambano hilo kocha huyo alisema kwamba
anaamini kuwa kikosi chake kitaweza kujirekebisha makosa na kucheza mchezo mzuri
utakaowapatia ubingwa.
Hata hivyo, alisema pamoja na kuwa Azam imeonesha kiwango kizuri lakini ana imani vijana wataweza kutoa ushindani na kuweza kushinda mchezo huo.
“Mchezo utakuwa mgumu kwa vile Azam imeonesha kiwango kizuri katika mechi zake zote lakini napendelea zaidi kombe libaki nyumbani,” alisema.
Naye kocha wa timu Azam, Stewart Hall ameahidi kuendeleza ushindi katika mchezo huo na kuweza kutwaa ubingwa.
Jumla ya timu nane zilikuwa zikishiriki michuano hiyo ambazo ni Yanga, Simba, Azam FC, Jamhuri, Mafunzo, Miembeni United, KMKM na Kikwajuni.
Search This Blog
Thursday, January 12, 2012
AZAM KUENDELEZA UBABE WAKE LEO DHIDI YA JAMHURI? MAPINDUZI CUP FINAL.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment