Mara soccer academy ilianza 8/2/2011 ambapo tulikusanya vijana 70 na kuwafanyia clinic ,tukapata vijana U 16- na wapo wadogo zao wengine U 12 kwa kushirikiana na Kamanda wa polisi Mara ACP Robert Boaz chini ya polisi jamii, tunao makocha 3 Ezekiel King Mbasa Kiumbe, na Mzee Msakato Magai ambao wanajitolea , vijana wanajifunza usafi binafsi, mbinu za soka, na wanajengwa kisaikolojia, jeshi la polisi wanafundisha watoto/vijana hawa juu ya sheria na kuwajengea uwezo kuepuka vitendo vya uharifu kama madawa ya kulevya, pombe , ubakaji na ukataji watu/upolaji, pia hutoa misaada ya usafiri wa vijana kucheza na timu za jilani au nje ya musoma.
mafanikio
-mradi umewatoa vijana ktk mazingira hatarishi
-85% ya mechi kadhaa walizocheza wamefanikiwa kushinda na zingine walidraw au kupoteza ambapo wamezawadiwa pesa taslimu, jezi, mipira lakini kubwa zaidi ni kujenga mahusiano mazuri na jamii
- kwa kushirikiana na Jeshi la polisi - Mara tumefanikiwa kuwatoa vijana ktk uharifu kwa 65%mfano ubakaji ukwapuaji, kamali , ugomvi na ukataji watu mapanga/visu ambavyo vilikuwa common Musoma ambapo kulikuwa na makundi hatarishi kama Mbio za vijiti, mdomo wa furu, jamaica mokkaz, jitume ,ffu yote yakihusishwa na uharifu
malengo: tunategemea kushiriki mashindano ya rollingstone-Arusha 2012 ili mkoa wetu wa mara uwakilishwe vyema na tayari tumeanza kujifua vilivyo, mkoa wetu hauna timu ya supa ligi hivyo tunategemea baada ya miaka 2 kituo hiki kitoe mchango mkubwa kuinua soka la Mara
changamoto
-uhaba wa dawa za michezo, vifaa bado havijakidhi mahitaji halisi,usafiri wa uhakika ili vijana wasafiri nje ya Musoma-
- vijana wote bado wanatokea majumbani, ila ingependeza kitafutwe kituo chao ili wakae pamoja na wapate diety inayoendana na mahitaji ya mazoezi ya soka na usafiri wa kuwapelekashuleni na kuwarudisha kituoni
wito
-tunawaomba wenyeji wa Mkoa huu wa Mara hasa Makongoro Mahanga, Gaudensia kabaka, Mzee wetu Warioba, Joseph Butiku, , Chacha Maginga , Charles Wambura na wadau wengine msogee karibu na misaada ya hali na mali ili Mara ipate heshima na vijana wetu tuwaendeleze wazifikie ndoto zao
Idara ya vijana na michezo na TFF watufikie na watujengee uwezo.
No comments:
Post a Comment