Timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Taifa Ngorongoro Heroes wametoka sare na mabingwa watetezi wa kombe la vijana la COSAFA, Zambia, mchezo uliochezwa katika jiji la Gaborone, Botswana.
Katika mchezo huo Ngorongoro wakishiriki kama timu mwalikwa walikuwa wa mwanzo kufungua ukurasa wa magoli kupitia kwa mshambuliaji hatari wa Azam Academy Msuvan HappyGod katika dakika ya 5 ya mchezo.
Goli hilo la Happygod lilidumu kwa mda wa dakika 5 na mnamo dakika ya 10 Evans Kangwa alisazisha goli hilo akiunganisha krosi ya Reynold Kampamba.
HappyGod alirejea tena kwenye nyavu katika dakika ya 25 lakini goli hilo lilidumu kwa dakika 3 pale Kangwa alipowasawazishia Wazambia kwa mkwaju wa penati kufuatia kuangushwa kwa Kampamba katika eneo la hatari.
Katika dakika 41 Ngorongoro walijipatia goli la 3 kupitia kwa Hassan Kessy na mnamo dakika ya 44 HappyGod alishindwa kuiandikia goli la 4 Ngorongoro na kujipatia Hat-trick na kupelekea timu kwenda mapumziko kwa Tanzania (Ngorongoro) kuwa mbele kwa goli 3 dhidi ya 2 ya Zambia.
Zambia walisawazisha tena katika dakika ya 84 kupitia kwa Alex
Sichone na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 3-3.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo la C ulishuhudia South Africa wakiwachapa goli 4-0 Mauritius, Na kushika usukani wa kundi hilo.
Search This Blog
Saturday, December 3, 2011
NGORONGORO WAANZA NA DROO COSAFA CUP
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment