Search This Blog

Wednesday, December 14, 2011

John Bocco: 'Huwa nafunga mabao ya Kuvutia'

MSHAMBULIAJI chipukizi wa Azam FC na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) John Bocco, ni mmoja ya washambuliaji ambaye mashabiki wengi wa soka nchini ‘hawamkubali’ kivile kutokana na aina ya mchezo wake wa taratibu.
Lakini pamoja na mtazamo wa mashabiki, hali ni tofauti anapokuwa katika klabu yake ya Azam FC, kwani ni mmoja ya wachezaji kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo. Bocco amekuwa akifunga mabao muhimu kwa timu yake hiyo tena hata dhidi ya timu za Simba na Yanga.

Mshambuliaji gani unadhani ni bora zaidi kuwahi kucheza naye timu moja?

Bocco: Washambuliaji wote niliopata kucheza nao niliwaona wazuri, sijaju ni kwa sababu ya ‘type’ yangu ya uchezaji kwa sababu nimecheza na washambuliaji wengi wenye aina tofauti na mimi na nimekuwa nikiendana nao, kwa mfano Yahya Tumbo na hivi sasa Ramadhani Chombo “Redondo”, Mrisho Ngassa na Amal Simba wote wapo poa tu.



Kocha gani bora zaidi kuwahi kufundishwa naye?

Bocco: Makocha wengi walionifundisha wamenijenga sana na siku zote nawaona bora sana kwangu, kwani toka nilipotoka chini naamini wao ndiyo siri ya mafanikio yangu haya ya sasa, kwani wengi walinijenga ili niwe mshambuliaji wa kati na si wa pembeni na makocha wote wananitumia hivyo. Pia wananipatia vitu tofauti na vya kisasa zaidi.

Bao gani ambalo ni bora zaidi umewahi kulifunga?

Bocco: Nimekuwa nikifunga mabao mengi mazuri kama unafuatilia mechi zangu utagundua hilo na mabao ninayofunga ni yale yanayofungwa na washambuliaji asilia. Msimu uliomalizika nilifunga mabao ya kuvutia sana na hakika ulikuwa msimu bora kwangu.




Ipi unadhani ilikuwa mechi bora zaidi kwa upande wako?

Bocco: Kila mechi ilikuwa bora sana kwangu kwani kila ninapokuwa uwanjani nawaza kuipatia timu yangu ushindi; ni zile nilizofunga ndizo zilikuwa mechi bora zaidi kwangu kwa sababu malengo yangu yalitimia.

Kikosi gani bora ambacho uliwahi kukichezea?

Bocco: Kwa kweli kikosi cha Timu ya Taifa (Taifa Stars) na timu yangu ya Azam FC, kwani siku zote huwa tuna kikosi bora sana, ukweli huwa nafurahi nikiwepo katika timu hizi mbili.

2 comments:

  1. Shaffih,yaani unproffesional players utawajua tu,sasa huyu bocco hata kujibu maswali hawezi,kila kitu anajibu too general na wala haileti raha,wenzao mbele wanahojiwa kwenye tv za club mpaka kwenye twiter na face book live na wanajibu straight hawaboi,huyu kila kitu anajumlisha what a pathetic,wajifunze kwa wenzao,hata mechi kali usikumbuke kaka,kocha eti wote wamekujenga then no tofauti au?rubish. chela wa dom

    ReplyDelete
  2. this is shame, huyu jamaa hawezi kufanya interview. au anaogopa lawama? maswali anajibu kiajabu ajabu tu kama vile anaogopa mtu flani atamlaumu kwanini hukunitaja vile aaaaagh too much bwana

    ReplyDelete