Nikikiona kikosi hiki hakika namkumbuka mtangazaji maarufu wa RTD wakati huo marehemu Dominic Chillambo,ambae alikuwa anatangaza soka la wa TP Lindanda kwa raha zake zoooooote, na ukisikia tu anavyoanza kutaja ile line up tu, akitaja kila jina moja mara mbili, mfano naaaaambari moja ni Paul Rwechunguraaaa, kisha atarudia tena Paul Rwechungura ni naaaambari moja, ...Je wewe unakumbuka nini hapa...hebu ntajie kikosi hiki kilichotesa miaka ya mwishoni mwa 80 hadi kati mwa miaka ya 90!
dah simchezo hichi kikosi ndiyo kilichoipa ubingwa malindi sports club kwa taabu sana 1989
ReplyDeletewaliosimama nikianza na kushoto wa computer yangu
ReplyDelete1;madata lubigisa
2;
3;beya simba
4teze john lungu
5;kitwana selemani
6;fumo feliciani
7;paschal mayala
8;poul rwechuguraaaaa
waliokaa chini kuanzia kushoto
1;george gole(shagh shagh)
2;alfhani gassa
3;ali bushiri
4;alphonce modest
5;mao mkami
6;
7;
8;nico bambaga
ndo ninawafaham,kwani nakumbuka wakati huo sh 100,unaigia mpirani pale kirumba kaka,
ebu nisaidie kitu kimoja je TORRRRRREEEEEEEEEEEEEEE, anaweza kurudi liverpool fc,kwani tunamuitaji sana kipindi hichi na kk anaweza kumrudisha leta majibu shafff
Hivi hao waliokaa watatu kutoka kushoto sio Ali Bushiri? Kwakweli huyu jamaa alikuwa fundi na kama niyeye basi mpaka sasa ni fundi balaa.. tuko chama moja la mateterani moro!! Jamaa anatisha mieldfielder ya juu Mbwiga cha mtoto kwa huyu jamaa.
ReplyDeletesasa mbona mmemsahau Hussein Masha na George Magere Masatu,Abdallah Boli na Rashidi Abdallah . Beya Simba
ReplyDeleteBwn Faustine Buyamba umepatia list yote, chama la home hilo halijapata kutokea,best team ever hii ndio ilikuwa barca ya enzi hizoo, usifanye mchezo tatizo exposure, vision na maadalizi vilizuia kuwika kimataifa, balaa. hao uliowasahau namba 2. Rajab Msoma "Fundi" mtoto wa town huyo alikuwa anapiga midfield ukimcheki anacheza ka Deco vile...Namba 6. waliokaa Mohammed Saleh "Bronco" mtoto wa uswazi huyo Igogo mwembamba alafu mgumu kama chuma,
ReplyDelete