Mbio za kwenda Brazil zinaanza mwishoni mwa juma hili na kuna nchi zaidi ya 200 zitakua zinagombania nafasi 31 huku nafasi moja ikiwa tayari imeshachukuliwa na mwenyeji.
Ni kama mwezi tangu tumefungwa na Morocco katika mechi ya mwisho ya kufuzu CAF 2012, Tulienda Morocco tukiomba miujiza na kwa bahati mbaya miujiza haikutokea, ukweli ulionekana kwamba Morocco walikuwa wazuri kuliko sisi, Kocha wetu mkuu Jan Poulsen pamoja na wachezaji wetu walikiri wenyewe kuzidiwa kimpira.
Sasa tunaenda kuwakabili Chad hata kama tukifanikiwa kuwatoa kwenye hii raundi ya awali lakini bado tutakaokutana nao mbeleni ni hao hao Morocco pamoja na miamba mingine kama Ivory Coast kwenye hatua ya makundi.
Hivi ni kweli watanzania wangapi wanaoweza kujiangalia kwenye kioo na kusema wana imani na sisi kwenda katika fainali za Kombe la Dunia Brazil, Tuwe wakweli kwanza na Hatuweza kabisa kwenda Brazil kwani Itakuwa ni miujiza ya hali ya juu.
Sasa kama we Malinzi unatambua hilo, na we Tenga unatambua hilo na viongozi wote wa Serikali wanatambua hilo kwanini tunatumia kile kidogo tulichonacho katika kushindana kwenye mashindano ambayo tunajua hatufiki popote ? Kwanini umlipie Nizar Khalfan kutoka Canada,Henry Joseph,Abdi Kassim waje kujiunga na timu wakati tunajua hatuendi kokote?
Mheshimiwa Pinda, kwa nini uwahimize watanzania wasaidie kwa hali na mali timu yetu wakati sote tunajua hawawezi kwenda Brazil bila miujiza?
Tukubali kwamba 2014 hatuendi Brazil hivyo mtuondoe mzigo wa matumaini ya kufuzu kwa miujiza na Kwanini tusitumie kile kidogo kilichopo kujenga timu ambayo mategemeo yake hayatategemea miujiza kufuzu fainali za kombe la mataifa afrika na kombe la dunia katika miaka kadhaa ijayo.
Nafasi ya kujenga timu kama hiyo ipo, lakini kwa nchi masikini kama yetu hatuwezi kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja, inabidi tukubali moja na hamna muda mzuri kama huu kukubali kwamba nafasi pekee tuliyonayo ya kwenda kombe la dunia au hata kombe la CAN ni kwa kujenga timu mpya, tukitumia vijana wetu wadogo.
Lazima tujipe nafasi ya kwenda huko kwa uwezo wetu. Na njia pekee ni moja na haijabadilika katika swala la mpira. Njia pekee ni kujenga upya mfumo wa mpira wa Tanzania kuanzia ngazi chini.
Kwa wafadhili wetu NMB, SERENGETI na wengineo. Kama kweli mnapenda maendeleo ya mpira wa nchi yetu? Basi fanyeni maamuzi ya kibiashara maana kama wafanya biashara najua mtawekeza pale mnapojua kuna nafasi kubwa ya mafanikio. Invest for the future, italipa maana wapenzi wa mpira hapa tuko nanyi kwa muda mrefu sana, bia zenu tutazinywa bado na benki tutaweka hela zetu.
Msaada wenu kwa miaka ya karibuni imetusogeza sana mbele na tunawashukuru sana kwa hilo, lakini hapo ndio tumefika mwisho kwa vipaji tulivyonavyo, hata mkiongeza mara tatu mnachotoa.
Sisemi tusishiriki kwenye haya mashindano, nachosema tushiriki na timu zetu changa ili ushiriki wetu uwe kwa madhumuni ya kuwapa vijana wetu uzoefu (experience) sio kwa madhumuni ya kujaribu kwenda Brazil 2014 au CAN 2015…
TUSAHAU! TUSAHAU! TUSAHAU KWENDA BRAZIL 2014!! ITATUSAIDIA KUJIPANGA ILI TWENDE RUSSIA 2018 AU QATAR 2022 KWA KUTEGEMEA UWEZO WETU NA SIO MIUJIZA KAMA ILIVYO SASA.
kaka nakuunga mikono miguu kichwa vidole na hata maneno tatizo watanzania tumezoea kujiongopea wenyewe na viongozi wetu wanafanya kila kitu iwe sisa hosp siasa barabara siasa michezo siasa sasa unafikiri tutakwenda wapi juzi nilimsikia waziri mkuu pinda akisema atatoa milionui kumi kuisaidia hii timu nikajiulizxa sasa huyu muheshimiwa hizi pesa si angetoa tu kwa mambo mengine kwa nn kwenye hii timu amabayo haina matumaini yoyote ya kwenda sehemu naona kuna haja ya kufumua timu yote na kuingiza watoto ambao watatusaidia siku za usoni
ReplyDeleteShaffih umenena! kiukweli ulichosema ndo ukweli halisia,kama miujiza hata tukiipata nadhani kwa Taifa Stars hii tutashindwa kuitumia!! sasa hv imefikia hatua timu ya taifa inapoteza mvuto kwa wazalendo kama sisi.Ni maajabu mvuto kuwa kwa simba na yanga[vilabu]kuliko National Team.
ReplyDeleteHii ina maana kwamba hatuna jipya kwa sasa,kilichopo kama ulivyosema tuangalie michuano ya 2018 na 2022 basi.
Hapo kaka ukweli mtupu kuhusu soka letu,yabid tujipange kwanza na si kukurupuka,nchi kama Tz ina vipaji lukuki vya soka sema hawajawekewa mwendelezo,Wako wapi Serengeti Boys ilee ya akina Mgwao,Nurdin,Mangunguru etc nadhan mkazo ungeanza na timu ile saa hz bongo ingekua full $hangwe kaka.
ReplyDeleteHuo ndo ukweli kaka anaoupinga mchawi....
ReplyDeletemaisha yangu yote sijawahi kuona mpira ukiombwa kama kauli mbinu yetu "watanzania tuiombee taifa stars ishinde" mpira ni uwezo wala hauombwi, mathalani ukutane na kosi ambalo lina mafoward wafuatao, right wing c.ronaldo left wing silva halafu katikati kuna messi na mario Gomez, ni maombi gani yatakufanya usalimike wavu wako usitikisike? wote hawa wametoka team za vijana wamekuzwa, lazima nasisi tuwekeze kwenye team za vijana under 17 hadi under 23 kwa-program endelevu, la sivyo tutakuwa tunalia everyday, sawa na msemo wa mbiga, "kazi ya fundi cherehani ni kukata tuu hata ulete kitambaa cha suti za laki 2 yeye kabla hajashona ni wajibu wake kukata, tutakatwa sana hadi tubadilike!
ReplyDeleteTrue kaka
ReplyDelete