Kocha Josep Guardiola ameifundisha klabu ya Barcelona katika michezo 200 juzi usiku mjini Prague. Akiwa ni kocha wa tano wa Barca kufanikiwa kuiongoza timu kwa idadi hiyo. Lakini hakuna kati yao mwenye rekodi ya kushinda mechi nyingi kama Guardiola.
TAKWIMU
72% KUSHINDA: Katika mechi 200 , Barca wameshinda 143, wakidraw 39 na kufungwa 17.
Asilimia 72 za ushindi kwa Guardiola, anafuatiwa kwa karibu na Helenio Herrera, ambaye alishinda kwa 70% ndani ya michezo 143. Anayefuatia Ferdinand Duacik aliye na wastani wa asilimia 60.7 katika michezo 150, Frank Rijkaard 58% katika michezo 273 na Johan Cruyff aliye na wastani 58.1% ndani ya mechi 430.
TAKWIMU ZA BARCA CHINI YA GUARDIOLA
KUFUNGWA MECHI 17 TU: Kati ya mechi 200, Guardiola na wachezaji wake wamepoteza mechi 17 tu, mbili kati hizo walipoteza mwishoni mwa msimu wa 2008/09 kipindi ambacho tayari walishauweka ubingwa wa La liga kibindoni. Msimu huu Barca hawajapoteza hata mechi kati ya mechi rasmi 17.
MAGOLI 500: Katika michezo 200, Barca wamefungta magoli 500. Huu ni wastani wa 2.50 goals per game. Leo Messi pekee akiwa amefunga mabao 160, ni mfungaji bora ndani ya uongozi wa Guardiola.
MAGOLI 99 BARANI ULAYA: Barcelona wamefunga mabao 99 in 44 Champions league’s matches chini ya uongozi wa Guardiola, na msimu waliowafunga mabao mengi zaidi ukiwa wa 2008/09. (36 goals in 15 Matches).
WAMEFUNGWA MAGOLI 143: Defence ya Barca imeruhusu mabao 143 katika mechi 200(0.71 per game), kati ya hayo 84 yamefungwa katika La Liga na kumfanya kipa Victor Valdes kuchukua mara 3 mfululizo tuzo ya Zamora.
POINTS 306 KWENYE LA LIGA: Katika La liga ndani ya mechi 124, Barca wamefanikiwa kuchukua points 306. Guardiola alimaliza msimu yake mitatu ya mwanzo na Barca akipata pointi 87, 99 na 96, ambazo zilitosha sana kushinda mataji. Msimu tayari wana pointi 24.
MATAJI 12 KATI YA 15: Mechi 200 zilizokihusisha kikosi cha Guardiola kimeshinda mataji 12 kati ya 15 waliyoshindania. Matatu ya La Liga, 3 spanish supercup, 2 champions league, 2 European supercups, 1 Clubs World cup na moja la Copa de Rey.
No comments:
Post a Comment