Shirikisho la Soka Tanzania TFF, limewateua Charles Boniface Mkwasa na Jamhuri Kihwelo kuongoza jahazi la Kilimanjaro Stars kwenye Michuano ya Kombe la Chalenji inayoanza Novemba 25 hadi Desemba 10 katika miji ya Dar es Salaam na Mwanza.
Mkwasa amewahi kufundisha Taifa Stars miaka saba iliyopita, lakini kwa sasa amekuwa akiinoa timu ya soka ya wanawake ya Twiga Stars aliyoiwezesha kuingia Fainali za Afrika kwa wanawake zilizofanyika Afrika Kusini.
Pia aliiongoza timu hiyo katika Michezo ya Afrika iliyofanyika Maputo Agosti mwaka huu. Mkwasa pia anainoa Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 13.
Hatua ya uteuzi wa Mkwasa imekuja baada ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kutembelea TFF kukagua shughuli za taasisi za michezo ikiwemo Baraza la Michezo la Taifa, BMT na TFF.
Chini ya Makamu Mwenyekiti wake, Juma Nkamia aliitaka TFF kusaka kocha mwingine kwa ajili ya Kilimanjaro Stars kwenye michuano ya Chalenji kwa kuwa itakuwa haitendei haki Zanizbar ambayo wachezaji wake wanakutana na Poulsen kwenye Taifa Stars.
Kamati ilisema kuwa ni vema Poulsen aliyeipa Kilimanjaro Stars Kombe la Chalenji mwaka jana, akabakia kuwa kocha wa Taifa Stars kwani inaweza kuzua mgogoro kati ya ZFA na TFF. Zanzibar ilipinga hayo mwaka jana lakini TFF 'ilikomaa' na kumwacha Poulsen kuendelea na kibarua Kilimanjaro Stars.
Osiah alisema Kamati ya Ufundi ilikutana pamoja na mambo mengine ilijadili suala hilo na kufanya uamuzi wa kuwachagua makocha hao huku Kihwelu akiwa kocha msaidizi.
Alisema kamati imewateua makocha hao kutokana na uzoefu walionao na Kamati ya Ufundi ina imani kuwa watafanya vizuri katika kuhakikisha timu inatetea vema ubingwa wake. Meneja wa timu hiyo ni Khalid Abeid.
"Kamati ya Ufundi imewateua na wamepewa kila jukumu ikiwemo kutaja kikosi timu itaingia lini kambini itafanyia wapi mazoezi na mambo yote kuhusu timu hiyo," alisema Osiah.
Charles Boniface Mkwasa na Jamhuri kiwelu.watu wawili wenye zengwe sana katika soka,watakutana na Mzee wa kubana Sunday kayuni.Team itatoka Dar-es -salaam na wale aliowakataa Mzungu lazima wawepo.Mipango Hasi
ReplyDelete