Search This Blog

Monday, November 28, 2011

LIGI KUU YA ENGLAND KWENYE NAMBA -JOHN TERRY MLINZI ALIYEFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE EPL.


2: Swansea City wameruhusu magoli mawili tu katika uwanja wao wa nyumbani msimu huu, idadi ndogo zaidi katika Barclays premier league.

4: John Terry amefunga magoli manne msimu huu, magoli mawili zaidi ya walinzi wote katika epl.

5: Wolves sasa wamepoteza mfululizo mechi tano za ugenini, baada ya kufungwa na 3-0 na Chelsea.

5: Liverpool wanabakia kuwa unbeaten katika uwanja wa Anfield lakini sasa wamedroo mechi tano baada ya kutoka sare na City.

6: Golikipa wa Swansea City Michel Vorm sasa amefanikiwa kupata clean sheets 6, zaidi ya kipa yeyote kwenye epl msimu huu.

11: Sergio Aguero amekuwa akifanyiwa substitution katika mechi 11 za EPL ambazo alianza msimu huu. Idadi kubwa kuliko mchezaji yoyote msimu huu.

19: Japokuwa walipata sare ya 1-1 @Old Trafford, Newcastle hawajaifunga Manchester United katika majaribio 19.

26: Fulham hawajawahi kuifunga Arsenal kwao. Droo waliyopata ya 1-1 at Emirates Stadium ndio ilikuwa mechi yao ya kwanza kupata japo pointi kotoka kwa Gunners katika mechi 26.

28: Ushindi wa Tottenham wa 3-1 dhidi ya West Bromwich Albion uliwafanya kuifikisha pointi 28 kutoka 30 walizotakiwa kupata tangu walipopoteza mechizao mbili za ufunguzi.

535: Kabla ya kifo chake, Gary Speed alicheza katika mechi 535 za ligi kuu, mchezaji wa tatu nyuma ya Ryan Giggs na David James.

No comments:

Post a Comment