METHOD MOGELLA ( KUSHOTO ) AKITAMBULISHWA KWA MH JOHN SAMWEL MALECELA NA ZAMOYONI MOGELLA
TAREHE 12/11/1994 MISHALE YA SAA SABA MCHANA MAENEO YA BUGURUNI JAY AMBE NYUMA YA ROZANA ALIYEKUA KIUNGO WA SIMBA NA TIMU YA TAIFA METHOD MOGELLA ' FUNDI ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUUGUA KWA MAJUMA MAWILI. HII ILIKUA NI SIKU YA MAAJABU KWA DADA YAKE MKUBWA ANGELINA MOGELLA WAKATI TAARIFA ZA MSIBA WA MDOGO WAKE ZINAMFIKIA GHAFLA ALIJISIKIA UCHUNGU WA MAMA MZAZI KWASABABU ALIKUA NA UJAUZITO, WAKATI FAMILIA YA MOGELLA IKIWA KWENYE HARAKATI ZA MSIBA, DADA ANGELINA ALIKIMBIZWA KWENYE HOSPITALI YA TMJ NA MNAMO SAA NNE USIKU ALIJIFUNGUA MTOTO WA WAKE WA TATU WA KIUME, MTOTO YULE ALIPEWA JINA LA METHOD ANICETH, ANICETH METHOD AMBAYE KWA SASA NI MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA AZANIA LEO ANATIMIZA MIAKA 17 YA KUZALIWA.
KWAHIYO LEO NI SIKU AMBAYO METHOD MOGELLA ALIFARIKI DUNIA NA BAADA YA MASAA 9 AKAZALIWA UPYA...
METHOD ANICETH ANACHEZA SOKA NA AINA YAKE YA UCHEZAJI NI KAMA MAREHEMU MJOMBA WAKE....
Keep't up method aniceth...
ReplyDeletesiku yako ya kuzaliwa ni muhimu sana kutokana na kumbukumbu ya Jembe la TZ ktk soka method mogellah!!
Nakutakia mafanikio ktk kuendeleza yale aliyofanya marehemu mjomba wako Method Mogella.Alikuwa ni fundi wa ukweli ktk kusakata soka.Nina magazeti nimeyatunza kwa miaka karibu 18 sasa kuhusu kifo chake...RIP Method Aniceth Mogella
ReplyDeleteHivi alikua mchezaji wa simba au yanga?wekeni kumbukumbu zenu sawa kabla ya kupublish wazee
ReplyDeleteHivi alikua mchezaji wa yanga au wa simba?!!!wekeni kumbukumbu sawa au nendeni pale tff mumuone kaimu katibu mkuu pale awapatie kumbukumbu kabla ya kupublish
ReplyDelete